6.3 C
London
Tuesday, December 10, 2024
HomeCommunityMatatizo ya Ushuru wa Nyumba

Matatizo ya Ushuru wa Nyumba

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes


Ushuru ni Hali Hela ambazo watu hutozwa ili kujenga Taifa.kila mkenya ana jukumu la kutoa ushuru katika serikali za Kaunti au za kitaifa , pindi tu baada ya uchaguzi mwaka wa elfu mbili na ishirini na tatu.mambo mengi yalibadilika nchini Kenya.Rais William Ruto alitangaza kuhusu makato ya ushuru wa nyumba za Bei nafuu.

Unapotembea mjini au barabarani utawapata wakenya wengi wanajiuliza maswali mengi kuhusu ushuru huu wa nyumba. Je, nitapata nyumba ikiwa nitalipia nyumba za Bei nafuu? Je ikiwa tayari Nina nyumba? Ni muhimu kulipia nyumba za Bei nafuu, jawabu ni kuwa suala hili ni lazima na Rais amepitisha ili iwe ni Sheria rasmi nchini kenya . Wakenya wengi hawana furaha kuhusu Sheria hii.

Inadaiwa kuwa wabunge walipitisha Sheria hii kwa kupiga kura bungeni , bila kufahamu inahusu nini.wengi wao wanajutia Sheria hii ya kutilia shaka mno. Ilikuwa ni Sheria kubwa kwa wabunge wa kenya kwanza baada ya Sheria hii kupitishwa kila bungeni kuwa sheria.hata seneta wa Busia bwana okiya omtata alielekea mahakamani ili kupinga Sheria hii kwa mapana na marefu .kesi hii iliwasilishwa katika mahakama nchini kenya.baada ya kuhakikisha kesi hii okiya omtata alikuwa mashuhuri sana, halafu akatoa madai kuwa maisha yake iko hatarini, kwasababu anapinga Sheria hii, jambo hili lilimtia wasiwasi mno lakini hakulegeza misimamo wake kuhusu Sheria yenye utata. Ni wazi kuwa kesi hii ilikuwa na ushahidi wa kutosha. Lakini mahakama ilifutilia mbalimbali ushahidi huu, na kulifanya kuwa Sheria.

Ilikuwa siku ya Jumatatu tarehe kumi na nane machi ambapo Rais William Ruto alitia sahihi mswanda huu kuwa Sheria nchini kenya.Ni wazi kuwa wakenya wengi hawana ufahamu kuhusu Sheria hii kamwe.kila mmoja anahitaji kukatwa pesa kila mwisho wa mwezi kugharamia Sheria hii .watu wote walioajiriwa katika serikali sasa watakatwa mashahara.Rias alisema kuwa waendeshaji wa pikipiki watakatwa pesa kulipia ushuru huu wa nyumba.bwana David hinga katika mahojiano na runinga ya citizen anadai kuwa ni lazima mikakati iwekwe ili wale ambao hawana ajira katika serikali pia wagharamia ujenzi wa nyumba.

Katika mradi wa nyumba rais William Ruto anadai kuwa Nia yake ni kufuatia vijana kazi kupitia kwa ujenzi wa nyumba.kama tujuavyo nchini kenya hakuna kazi .Kuna baadhi ya vijana wamefuzu kutoka chuo kikuu , lakini bado wako mtaani bila ajira kamili. Rais William Ruto anadai kuwa kazi za ofisi ni vigumu kutapa kwa urahisi.katika ujenzi wa nyumba ya gharama nafuu. Mama mboga ataweza kupata ajira wakati ameanda vyakula kwa wale wajenzi wa nyumba.vijana wengi watapatiwa kazi ya kujenga nyumba hii. Marehemu kelvin kiptum alijengewa mfano wa nyumba, ambayo ni mojawapo wa nyumba za Bei nafuu. Kuna waandishi ambao hufanya kazi hii. Naibu wa Rais bwana Rigathi Gachagua anadai kuwa yeye Hana kazi ya kuwapatia vijana mtaani. Lakini kupitia ujenzi wa nyumba za Bei nafuu vijana wataweza kupata ajira.wabunge wa kenya kwanza wamepigia debe Sheria hii katika mkutano wa kisiasa.

Mnamo januari mwaka wa elfu mbili na ishirini na nne nchini kenya wabunge walipendekeza marekebisho katika mswada wa fedha huu ni kinyume na katiba na kuwaaambia waajiri wasilipe au kukubali kukatwa pesa hizo.Rais William Ruto katika serikali yake anandoto ya kukusanya shilingi 63.2 billion mwaka wa kifedha wa Juni elfu mbili ishirini na nne.

Ni jambo la kutia aibu mno kwa kuwa baadhi ya watu ambao waliachwa nje ya mpango huu lazima watawekwa kikamilifu.kwa hivyo mpango huo utapokea michango zaidi kiliko awali.sheria ya mswada wa nyumba inabainisha kuwa mtu mmoja anaweza tu kununua kitengo Cha nyumba moja, Kisha Wala ambao hawawezi kupata nyumba wanaweza kutuma maombi ili waweze kuondolewa kwenye akiba hiyo.

Waziri wa ardhi nchini kenya bi Alice wachome Naye alisifia nafasi za ajira zitakazopatikana kutokana na ujenzi wa nyumba hizi za Bei nafuu. Wakenya bado wanazidi kufa moyo kila siku , naye naibu wa Rais wa Rigathi Gachagua anadai kuwa mpango huo wa nyumba za Bei nafuu utafaulu, katika serikali ya kenya Kwanza mradi muhumu zaidi ni ujenzi wa nyumba za Bei nafuu. Watu wengi nchini kenya wamebomolewa majumba Yao. Kama vile katika kaunti ya Bungoma, Mombasa na hata Nairobi.wakenya wengi wanalalamika kwa kuwa wamepoteza makazi Yao . wakenya zaidi wa mapato ya chini wameweza kujipatia kipato kwa njia tofauti katika mradi wa ujenzi wa nyumba hizi nafuu. Si ajabu kufahamu kuwa Rais William anadai zaidi katika kuboresha Sheria za ujenzi wa nyumba ya Bei nafuu zaidi.

Mswada wa nyumba ilitiwa sahihi katika ikulu ya Nairobi. Ni wazi kuwa kutiwa Saini kuwa Sheria hii kunamaanisha kuwa ushuru wa asilimia 1.5 kwa mapato ya wafanyikazi kote nchini umerejea au kurudi .waajiri na waajiriwa walichangia shilingi 26.8 billioni chini ya ushuru wa nyumba uliozua utata . Wakenya wanalia kuwa gharama ya maisha imekuwa juu zaidi kwa hivyo wanamwomba Rais William Ruto kufutilia mbali Sheria hii, ingawa vijana watapata kazi , lakini Bado , Kuna utata kuhusu makato zaidi.Ni vyema Rais kuwa punguzia wakenya mzigo zaidi.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img