7.6 C
London
Friday, October 11, 2024
HomeEducationUMUHIMU WA MICHEZO

UMUHIMU WA MICHEZO

Date:

Related stories

How Can African Women Bridge the Digital Gender Gap?

By Guest Writer There is a harsh reality in digital development:...

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...

Vumbi Ni Hatari Katika Afya yetu?

Vumbi ni hali ya chembe zinazopeperuka hewani za asili...

Fahamu Zaidi Alama Za Barabarani

Alamu za barabarani huweza kuwa nguzo muhumu kwenye kando...

Hofu Yatanda Kufuatia Mlipuko Wa Mpox

Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya "Monkey Pox"...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes


Mzazi anapompeleka mtoto shuleni ana matumani chungu nzima. je, atakuwa rais wa nchi au mwanasheria? Haya yote Huwa maswali ya wazazi huko Kijijini. Talanta Huwa kipaji Cha kupatiwa na mwenyezi Mungu. Si kila binadamu atakuwa daktari wa mifupa au upasuaji , kupita riadha faith Kipyegon aliweza kujulikana si afrika pekee Bali hata pembe zote za Dunia. Sifa zake zilisambaa kama kichaka kilichowaka moto. Sifa hizi zilimpatia heshima na kufahamika kote duniani.

Faith Kipyegon aliweza kutunukiwa na rais William Ruto . Akiwa mwanafunzi yeyote alitia bidii ya mchwa darasani , bila shaka akafaulu na kupita mtihani wake. Mwanariadha huyu hakulaza damu Bali alitia bidii Kisha ndoto yake ikatimia.
Wakati unatia bidii jambo Fulani, ni wazi kuwa utakuwa mfano Bora katika jamii . Mwanamuziki bahati alitia bidii kwa sasa yeye ni mwanamuziki hodari. Wale vijana ambao walikuwa na uoga , sasa wamekuwa jasiri . Nani angelifahamu kuwa linet toto, angekuwa mwakilishi wa kinamama huko gatuzi la bomet? Habari za mjini ni kuwa bidii hulipa. Vijana wameamini kuwa ukitaka kufaulu lazima usisahau kujaribu , jambo hatimaye utafaulu maishani.
Baada ya kuishi katika umaskini kwa muda mrefu .maisha ya faith Kipyegon iliangaziwa baada ya kushinda Kisha akatangazwa kwenye runinga.ndoto yake faith ilingaa wakati raisi William Ruto alimzawidi na jumba la kifahari . Kwa kweli Talanta hulipa . Ilikuwa ni furaha kwale faith kwasababu hakuamini atabadilika na kuwa tajiri hitajika.

Pesa ni sabuni ya roho. Ukiwa na pesa kila jambo Huwa rahisi kufanya. Kila mtoto Huwa na furaha zaidi akitembea na kuzuru sehemu mbalimabali kama vile mbuga za wanyama. Mtoto wake faith aliweza kupelekwa kule Canada kwenda kujionea madhari kama njia moja ya kumpumzisha akili baada ya kufunga shule.
Utangamano katika nchi ni jambo la muhimu zaidi . Je, unafahamu utangamano ni nini? Utangamano ni Hali ya hali ya kuwa na usawa katika jamii na Hali kuisha kama familia moja. Kupitia ushinda wa faith ilimfanya kuwazungu na kujulikana kote duniani. Pia ushindi wake ulifanya kenya kujulikana duniani faith alipotangazwa kuwa mshindi.
Bingwa huu wa riadha alijawa na furaha , baada ya shirika kuu la ” Safaricom kumpatia baba yake gari. Ingawa faith alikuwa na ndoto ya kumnunulia baba yake gari. Baada ya kushinda na kuwa nambari moja, matumani ya baba yake kupata gari jipya ilitimia .

Bali na mchezo wa riadha , Kuna aina mbalimabali za michezo Kama vile kandanda , voliboli , karate , mpira wa kikapu na mengineo. Mchezo Huwa muhimu zaidi ni njia moja ya kujenga mwili.
Michezo ni muhimu sana na hufanya vijana kuwa na Talanta mbalimbali, kwa mfano Julia’s yegon alikuwa na umaarufu wa kurusha mkuki. Michezo hufanya vijana kusahau kunywa pombe kule Kijijini pia mwanandondi maarufu conjestina Achieng alijulikana kupitia Talanta yake. Wakati alikuwa mgonjwa, ilikuwa rahisi kusaidiwa na aliyekuwa Gavana wa Nairobi mike sonko , conjestina alipelekwa mjini Mombasa na kupewa matibabu.

Gavana wa migori Gladys wanga , kila mara anapenda kandanda. Ni jambo la kufurahisha hata yeye binafsi hukimbia. Timu ya gor mahia haingekuwa na mashabiki wengi, ikiwa watu wengi hawapendi michezo. Asiyekubali kushindwa si mshindani , timu ya police imewashinda timu ya gor mahia mabao tatu kwa sifuri. Ingawa uchumi imekuwa mgumu . Mashabiki waliweza kulipa shilingi elfu tatu ili kutazama mechi.

Timu ya wasichana ya Harambe starlets ilitia bidii kuwasilisha wakenya kule Botswana. Wasichana waoliowakilisha timu hii , walikuwa wakichezea timu za humu nchini. Kandanda ni Talanta ambayo hulipa zaidi. Wachezaji hao wameweza kuwasomesha na kusaidia familia zao. Ni jambo la kufurahisha timu ya Harambee starlets wakicheza na Botswana hapa nchini matokeo Yao ikiwa ni sare . Waliposafiri Botswana pia walitia bidii, lakini Botswana walishinda kwa mabao mbili kwa moja. Hongera harambee starlets kuwasilisha nchi yetu . Kocha belden alijaribu uwezo wake lakini hatimaye hakufaulu matokeo Bora .

Ni matumani yangu kuwa serikali ya kenya itazidi kuwatia moyo wachezaji Hawa ili wasife moyo. Katika kaunti ya Kisumu . Kulikuwa na mchezo wa kandanda. Ilikuwa furaha tele “Cecafa” iliwavutia mashabiki wengi zaidi. Timu nyingi za Afrika zilishiriki kama vile Uganda, Sudan , Tanzania na mengineo. Watu walijaa kaunti ya Kisumu . ” Harambee star junior” ni vijana ambao hawajahitimu miaka kumi na nane. Wakenya walikuwa na matumani kushinda kikombe Cha “Cecafa” ajabu ni kuwa waganda ndio walishinda .
David Rudisha na Lilian Obiri pia wameonyesha umaarufu wao kupitia michezo. Ni jambo la kufurahisha kuwa David Rudisha amejenga shule na pia viwanja . Watoto ambao walikosa Karo pia aliweza kuwalipia. Hongera kwa mwanariadha mashuhuri Lilian Obiri kwa ushindi wako. Michezo ni jambo linalofanywa kwa ajili ya kushindana , kujifurahisha, kujichangamsha . Pia husaidia kuimarisha afya ya mwili , ubongo na akili.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img