19.5 C
London
Monday, July 15, 2024
HomeCommunityJANGA LA UKAME NCHINI KENYA

JANGA LA UKAME NCHINI KENYA

Date:

Related stories

Kenyan Police in Haiti Receive Armored Vehicles and Choppers to Combat Gangs

Kenyan police officers who are fighting gangs in Haiti...

Kenya on High Alert as Monkeypox Outbreak Spreads in DRC

In response to the rapidly evolving monkeypox situation in...

Kenyan Sensation Faith Kipyegon Shatters Own 1,500m World Record at Paris Diamond League

World 1,500m and Mile Record Holder Faith Kipyegon Secures...

Kenya unrest: the deep economic roots that brought Gen-Z onto the streets

By XN Iraki The generation of Kenyans born between 1997...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Ukame ni janga la asili ambalo hakina mtu anayeweza kuzuia kuja, lakini tunaweza kujiandaa kwa athari za janga hili la asili ili kufanya iwe ngumu kidogo. Hali ya hewa imebadilika sana kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira yetu. Vipindi virefu vya kiangazi navyo vimeanza ukame. Wakulima na wafugaji sasa wamesalia kukadiria hasara. Aghalabu ni milimani kwa misituni tu kunakonyesha mvua ya kutosha.

Hata hivyo ukame umeathiri sehemu mbalimbali humu nchini kama vile watu kumi wamefariki kule turkana kutakana na uhaba wa chakula . Isitoshe zaidi ya watu 800, 000 wakiendelea kutumia kwa makali ya njaa na kiu . Si ajabu kusikia katika Kijiji Cha ” kakwanyang” eneo la turkana ya kati mizoga ya wanyama iliyotapaka ni ishara tosha ya ukame . Ni jambo la kushangaza sana wakazi wa Kijiji hiki hawajatia chakula mdomoni kwa muda wa siku Tano zilizopita.

Ukame imeweza kusababisha njaa, magonjwa na hata vita, ni Bora kufahamu kuwa ukame unaweza kuwa na madhara makubwa ya afya kijamii , kiuchumi na kisiasa . Ukame unatokea pia pale ambako watu wa kilimo wanategemea maji kwa umwagiliaji na vyanzo vingine vya maji . Vimekauka .jamii hufunga safari moja kwa moja ili kutafuta maji ya kunywa.
Mamilioni ya watu huumwa au kufa kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira. Ukame hufanya shida kuwa mbaya zaidi . Wakati ukame ni mkali na unaendelea kwa muda mrefu , njaa inaweza kutokea kwa urahisi sana.

Ukame umesababisha vifo na kupunguza uzazi, ambayo ni shida hasa kwa wakazi wa aina za hatari ambao nambari zao tayari ziko chini mno. Wanyamapori pia huathiriwa na ukame na hatimaye hufa.
Matumizi mabaya ya ardhi husababisha kupunguza kwa mimea . Ardhi inakuwa wazi bila chochote na bila shaka Haina Kinga. Hali hii huongeza ukame wa ardhi. Mwishowe jangwa maeneo makubwa ya ardhi iliyoharibika . Binadamu atakosa chakula na pia maji . Kila mara ukame unapobisha hodi, Maisha ya wakazi na mifugo wao Huwa hatarini.

Jamii Huwa na migogoro , wakati bidhaa muhimu kama maji hukosekana. Ukosefu wa maji hufanya chakula kupotea , jambo hili hufanya watu kushidhana na hatimaye kupigana na kuuana, ikiwa kutakosa usalama wa kutosha jamii moja inaweza kuleta chuki na uhasama kwasababu ya maji.
Waziri wa utali na wanyamapori nchini kenya peninah malonza alieleza kwamba ukame umesababisha vifo vya wanyamapori Kumi na nne wameathiriwa zaidi. Ni vyema kufahamu kuwa ukame huu ni mbaya . Katika miaka arobaini zilizopita, ukame wa mwaka elfu mbili ishirini na tatu ilikuwa hatari zaidi.

Maenea ya kaskazini na kusini mw kenya ambayo tembo wengi hupatikana ndiyo yameathiriwa na ukame. Ili kuzuia janga hili ni Bora wanyama Hawa wapewe chumvi ya kulamba pamoja na chakula Cha kutosha. Utapia mlo unazidi kuongezeka . Utapiamolo ni Ugonjwa unaowapata watoto kutokana na ukosefu wa viinilishe vya kutosha katika chakula . Kaunti ya kaskazini mashariki mwa kenya athari ya ukame inazidi kuleta shida. Daktari mkuu katika hospital ya wajir kaskazini mashariki mwa kenya amethibitisha ukweli huu.

Ukame ya muda mrefu uimelazimisha familia kuondoka majumbani mwao kutafuta chakula na maji , na hivyo kuhatarisha afya zao, usalama na elimu . Sehemu kame zilipokea mvua kwa kiwango Cha chini mno. Katra Farah mtaalam wa lishebora katika shirika la ” save the children” , anasema imekuwa vigumu kwa familia nyingi baadhi Yao wakilala njaa au kupata mlo moja kwa siku. Watu wanaweza kuishi kwa wiki bila, chakula , lakini siku chache bila maji.
Ukame utapunguza kiasi Cha maji iliyohifadhiwa katika mabwawa . Kupunguza kiasi Cha nguvu zilizozalishwa . Jambo hili linawezaleta shida kwa jamii ndogo ndogo zinazotegemea maji machache , ambako taa ndogo ya umeme imewekwa.

Kuweka hatua ya mavumbi ambayo yanaweza kusababisha vifo pamoja na uharibifu wa Mali . Kwa jumla itaacha sehemu kuwa kavu. Chini ya unyevu na mvua ambao mara nyingi huonyesha ukame huleta Hali ya hatari katika misitu.
Katika kupambana na janga la ukame nchini , ni Bora kuuza mifugo wakati wa mvua na kuweka fedha ili kujinusuru wakati wa kiangazi , itasaidia pakubwa katika kuhakikisha kwamba ukame unatupiliwa katika kaburi la sahau.
Pia ni bora kueneza teknolojia za kukabiliana na ukame na kuunga mkono sera na hatua ambazo zitashawishi matumizi matumizi Bora ya ardhi na maji.ifahamike kuwa ardhi inaweza kutumika katika kilimo tena , ikiongeza usalama wa chakula na mapato kwa watu wengi katika jamii.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_img
Previous article
Next article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here