Maarifa ni uwezo wa kushinda au kupata kitu fulani unachotaka. Maarifa hufanya mtu kuwa na uwezo na akili wa kujua,jina, umaarufu wa mtu, nguvu, kiwango Cha pesa, cheo na hata vitu ambavyo anapenda kumiliki. Zaidi ya yote maarifa ndiyo nguvu kuu ulimwenguni. Ili kumtoa mtu katika shida lazima uwe na maarifa. SI ajabu lazima kutaja mambo teknolojia ambayo huhusisha maarifa zaidi, bali kushukuru watafiti kwa kufanya muujiza. Katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wahandisi wakitumia maarifa zaidi ili kujenga nyumba ya marehemu Kelvin Kiptum kwa siku tatu. Hii ni maarifa kupita kiasi.
Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa. Inawezekana kusema kuwa uchumi wa jamii ya leo unategemea maarifa zaidi katika masomo ya umilisi almaarufu “C.BC.” kuliko kutegemea serikali kuu ni bora kujifunza kazi za mikono ambazo huhitaji maarifa kama vile uchoraji, ushonaji na ukulima.
Maarifa huhitaji data, waigizaji kule viusasa hutumia maarifa kutunga nyimbo, kutangaza biashara yao na mwishowe wanapata riziki. Suala hili linaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa ya teknolojia kwenye tarakilishi. Maarifa huenea kwa haraka sana, si ajabu kufahamu kuwa maarifa yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya ishara. Ikiwa unataka kuendesha chombo fulani kutoka sehemu moja hadi nyingine, lazima uweze kuwa na maarifa, rubani hawezi kuendesha ndege ikiwa hana ujuzi, pia dereva huhitaji maarifa ili kuzuia ajali barabarani, nchini Kenya ajali barabarani ni nyingi sana usiku kucha, hii ni kwasababu ya ukosefu wa maarifa ya Kutosha kuzuia ajali.
Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa mfano kutembea, msingi na utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalishia maarifa mengi .Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyatambua .
Mtu ambaye amekosa maarifa fulani huwa amekosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huathirika.Maarifa huangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kutumia kwa faida yake au lengo la kuhifadhi jamii nzima.
Elimu ni chombo muhimu cha maarifa maishani.Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni za maarifa. Inawezakana kusema kuwa uchumi wa jamii za leo zijazo unategemea uwezo wowote mwingine. Kumbuka hata Yesu alijifunza poleple kwa muda. Ukosefu wa maarifa imesababisha vikwazo vingi kama vile umaskini, ushuru wa juu, migomo, ujinga na vita vya mara kwa kwa nchini. Watu wameweza kupoteza mali na rasilimali kama vile mifugo.
Ukosefu wa maarifa imewafanya vijana kutumia dawa za kulenya. Ingawa wao hutambua kuwa dawa hizi zina madhara mengi, kutokana na kiburi chao wao hutumia dawa hizi ili kufurahisha nafsi zao. Kutoka kaunti ya Mombasa dawa hizi zimekuwa tatizo,vijana wenye umri mdogo wamebadililika na kuwa majambazi sugu. Gavana wa Mombasa ametoa onyo kali kwa watoto hawa wanaojihusisha na uhalifu kuwa watatiwa mbaroni.
Hii ndio maana naibu wa Rais bwana Rigathi Gachagua anapigia upato vyuo vya kiufundi. Vijana wanahimizwa kujiunga na vyuo hivi baada ya kumaliza masomo yao ya sekondari. Kila binadamu huhitaji maarifa kutekeleza jambo fulani. Kuna baadhi ya taaluma ambayo huhitaji maarifa ya kujifunza, kama vile udaktari, ama kuwa mwalimu. Ujuzi Huwa husaidia jamii kuwa na maendeleo.
Hata hivyo ukosefu wa maarifa hufanya wengi nchini kukosa kufikia malengo yao kutokana na kutomaliza masoma yao. Subira ya vuta heri kwa hivyo ni vyema kujitoa ili ufaulu maishani. Ni bora vijana wafanye maamuzi sahihi maishani. Ukosefu wa maarifa husababisha kupotoka kwa maadili, kama vile kudanganya katika mitihani ya kitaifa. Hii ni kwasababu utawapata wanafunzi hulegeza damu, badala ya kutia bidii masomoni.
Nchini Kenya kumetokea migogoro ya ndoa, hii huleta fujo na hatimaye watoto ndiyo huumia zaidi. katika kaunti ya Busia Kuna mwanamke ambaye alikatwakatwa vibaya kwasababu ya kuomba mahitaji ya wanawe, ikiwa mumewe alikuwa na maarifa ya kutosha basi kisa hiki hakingefanyika. Je, kwa nini vijana hujihususisha na ndoa za mapema, Kila mzazi ana jukumu kumpeleka mtoto wake shuleni ili apate elimu, wanafunzi wanapokuwa shuleni wao hufuzwa mashauri na uelekezi, ukosefu wa maarifa huwafanya wao kuacha masomo na kuanza familia.Kisha wao hujuta wakati maji yamezidi unga na kulaumu wazazi wao.
Tusingoje wanasiasa kutuletea unga, leso na pia kofia ya bure, ni bora kumfundisha mtoto kuvua samaki kuliko kuvuliwa kila wakati. Mabadiliko ndiyo kitu ambacho hudumu milele, na kila mara ni lazima kama ibada. Utasikia kila mara baadhi ya majengo mjini Nairobi yameporokmoka, Kisha maafa yakatokea, watu wamepoteza maisha yao, hii inatokana ukosefu wa maarifa. Kila taaluma inahitaji elimu ya kutosha, ikiwa mwanafunzi atakosa maarifa bila shaka atakosa kujua mengi nyanjani. Bila maarifa jamii itakosa maendeleo.