15.2 C
London
Tuesday, June 17, 2025
HomeCommunityTaswira Ya Mitaa Duni Almaarufu "Slum"

Taswira Ya Mitaa Duni Almaarufu “Slum”

Date:

Related stories

Kwa Nini Kinadada Hupenda Vibanzi “Chips”

Vibanzi ni vipande vyembamba vya chakula vilivyokaangwa kwa mafuta....

Building a fairer, Healthier Societies

Understanding the Link between Equity and Health The pursuit...

The power of the community: Unity in Action

Communities are the bedrock of human society. From small...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Katika mitaa duni watu huishi kwenye vibanda. Wakazi wengi wanaelezea changamoto kubwa ni kupata lishebora, nafasi bora za elimu, maji safi pamoja na usalama wa kutosha.

Kuna faraja kubwa baada ya taasisi mbalimbali za kibinafsi kutoa elimu, makazi na hata huduma za kiafya kwa jamii ambazo baadhi ya wakazi wake hujikuta walijihusisha na dawa za kulevya. Mpango wa Serikali wa kujenga na kuimarisha mitaa duni nchini ambayo ni makao ya watu takribani millioni tano nukta tatu, watu wengi katika maeneo hayo wanatarajia kupata makazi bora, ikiwa huduma bora za kiafya zitaboreshwa.

Watoto yatima katika mitaa duni mbalimabali huishi kwenye vibanda ambayo vimetengenezewa katika Mabweni na madarasa ni hatua muhimu ya maendeleo katika mitaa ili kudumisha elimubora. Watoto wengi wametelekezwa na jamii zao. Vilevile kukiri kuwa yapo matatizo makubwa ambayo watoto hao hupitia. Kundi la vijana nchini Kenya wametayarisha filamu inayosimulia maisha katika mitaa ya mabanda wakitumia simu za mkononi.

Filamu hiyo inashirikisha waigizaji ambao wao hawajulikani sana nchini Kenya na wanatumia lugha ya mtaani ijulikanayo kama sheng. Robo ya idadi nzima ya watu wanaoishi mjini kote duniani wanakaa katika mitaa duni ambayo yana mazingira hatarishi huku hali ya maisha ikiwa yenye uhaba wa huduma muhimu. Siku ya makazi duniani huadhimishwa kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi wa oktoba kila mwaka ikiwa na lengo la kumfanya kila mmoja atafakari hukusu hali ya mji na kuendeleza makazi bora kwa wote. Siku hii ni ya kutoa nafasi kwa wakazi wa mitaa duni husika.

Kibera ni mtaa katika jiji la Nairobi ambapo watu hushi na kufanya kazi ndogo ndogo kama kuuza mahindi ya kuchemshwa, matunda, mboga na kadhalika.Baadhi ya watu hao kunao ambao hawawezi kufanya kazi yoyote. Hata hivyo watu wengi wameonyesha sifa mbaya dhidi ya mitaa huo wa kibera lakini tunafaa kumbukumbuka ya kwamba kila kitu kina uzuri wake.

Watu wengi katika mtaa wa kibera huwa wanafanya kazi mbalimbali ili kujimudu kimaisha. Isitoshe sio kupenda kwa wale walioko kwenye hii jinamizi la umaskini. Tunaweza kuwa na nia njema kuhusu mitaa kama hii ili tusiwe kama watu ambao wanasema lakini kufanya ni shida sana. Ajira ni Kikwazo kikubwa kwa wakazi wa kibera.

Umaskini ni jambo la kuzingatiwa katika mtaa wa kibera kwa maana ndio mojawapo ya shida ambazo zinawakumbwa wenyeji. Baadhi ya kazi ambazo wanazofanya ni kama uchuuzi, kuosha nguo za majirani ili kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine.

Wakazi kutoka mtaa huu huaminika na wageni kutoka nchi za ng’ambo .Ingawa kuna shida ya mavazi , chakula lakini ajira imechangia sana kueneza umaskini katika jamii kwasababu watu wengi hawana mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ndogo ili kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida.

Katika mitaa duni maji taka za kila aina na harufu mbaya haikosi kuwa.Mamia ya watu huishi katika nyumba za eneo duni hawana makazi. Mji wa Nakuru haujaachwa nyuma, ila matokeo yake yanashangaza.

Kusini mashariki mwa ziwa la Nakuru takribani kilo mita tano kutoka katikati mwa jiji, upo mtaa kwa jina shauriyako. Mtaa huu inaaminika na serikali ya kaunti ya Nakuru ambako nyumba zilizojengwa huko ni za aina moja tu.
Wakazi wengi hapa ni wale ambao walikuwa wakifanya kazi katika manispaa ya Nakuru kabla ya ujio wa serikali za kaunti nchini.
Mtaa wa shauriyako ina nyumba za rumu moja katika kila eneo, gharama katika mtaa huu si ghali mno, mtu yeyote wa kawaida anaweza kuishi katika mtaa huu vyema bila kutatizika na majukumu ya hela. Nyumba za bei ya chini hata kwa elfu moja utapata makazi.

Usalama katika mtaa huu unazua wasiwasi si haba, vijana ambo wameteka nyara mtaa huu wanahangaisha wakazi kila mara. Je, hali ya maisha ikoje kibera? Maji safi ni haba. Magonjwa yanasababishwa na ukosefu wa usafi yanaonekana. Wengi wanaisha katika makazi duni wanakosa huduma za kimsingi, ikiwa ni pamoja na umeme, maji barabara na matibabu.

Umaskini umekita mzizi korogocho huku zaidi ya asilimia sitini ya kaya zikikabiliwa na matatizo ya kiuchumi. Wakati huo huo, kibera imekabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile nusu ya makazi Ina vijana wengi ambao hawana ajira.

Kelele za mashine ya kuchomea vyuma na kugonga mabati. Kwa marekebisho ya magari ni jambo la kawaida katika mtaa duni. Mama mmoja Katika mtaa huu duni alidai kuwa ametafuta kazi muda mrefu bila mafanikio. Wanawake huoshea watu nguo ili wapate kipato cha siku. Walio karibu zaidi na ukingo wa bahari ndio maskini zaidi.

Watu wengi wanaishi katika mazingira duni na nyumba zao zikipitiwa na mfereji ya maji. Taka husukumwa na maji taka hadi kwa nyumba za watu. Ni vyema serikali kuboresha mitaa duni ili watu waishi kwa amani. Mtaa duni si bora kwa afya za watu.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img