6.7 C
London
Tuesday, December 10, 2024
HomeBusinessTechnologyFAIDA YA SIMUTAMBA

FAIDA YA SIMUTAMBA

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Rununu au rikono ni simu ya mkono. Pia huitwa simutamba . Uvumbuzi wa simutamba ni uvumbuzi ambao tunaweza kusema kuwa ni mkubwa sana katika Karne hii baada ya uvumbuzi mwingine kama wa magari na runinga , vifaa hivi vyote hutumika katika mawasiliano nchini kenya kwa idadi kubwa ya watu mjini na hata mashambani.

Simutamba ni suluhisho kwa matatizo mengi ambayo binadamu walikuwa wakikumbana nayo . Simu hizi zinatuwezesha kuwasilisha ujumbe muhimu kwa njia ya haraka mno . Hebu fikiria Kuna ambaye maishani mwake Yuko hatarini lakini inakubidi upige foleni ili uweze kupiga simu ya dharura.
Siku hizi mambo kama haya yamezikwa katika kaburi la sahau . Kutokana na uvumbuzi wa simutamba au rukono . Ujumbe wa haraka huweza kuwasilishwa kwa njia ya haraka , moja kabla ya uvumbuzi wa simutamba maisha ya watu yangepotea kutokana na kukosekana kwa mawasiliano Bora.

Simutamba ni suluhisho kwa wale wanaoishi mashambani ambako simutamba za wakati huo kawaida hazikuweko. Uvumbuzi huo umempa kila mwanadamu fursa ya kuwasiliana na yeyote si nchini tu Bali hata katika nchi nyingine. Mawasiliano hayo ni njia Bora ya kila mkenya kujuliana Hali kote nchini.
Huwezi kukosa kupokea ujumbe wowote eti kwasababu ulikuwa mahali Fulani. Hivi vidumbwasha huwekwa hata vikapuni unapoenda shambani au sokoni. Siku hizi unandishi wa barua ni nadra sana kwasababu ujumbe unaweza kuwasilishwa kwa kutumia simutamba. Rununu inatupatia fursa ya kutuma ujumbe kwa wakati huo mwafaka .

Rununu pia hutumika kama kifaa au chombo Cha kijiburudisha. Aina za rununu Zina michezo ya aina mbalimbali ambayo unaweza kucheza wakati wowote ule. Isitoshe unaweza kupata ujumbe kupitia njia ya mitandao kupitia rununu ambazo Zimetandawizwa kutoa hudumu hiyo.
Kumbuka baadhi ya simu hizi zina kamera. Mtu anaweza kupiga picha na kuhifadhi ili aweze kuitazama wakati wowote . Panapokuwa na kumbukumbu muhimu ambazo zinafaa kurejelewa kila mara. Si lazima mtu aweke kwenye vitabu vya kutumia picha.

Licha ya haya , simu hizi zina shajara mahsusi za kukumbusha iwapo unahitaji kuwa mahali popote na kile ambacho unahitajika kufanya. Heko kwa uvumbuzi huu kwasababu suala la kusahau kuhudhuria mikutano haipo Tena.
Matumizi ya simu za mkono , yaani rukono miongoni mwa wanafunzi yanachangia kudorora kwa masomoni. Wengi hutumia muda mrefu huku wakicheza michezo mbalimbali au kuwasiliana na wenzao kila wakati.
Hata wanapotumwa na wavyele wao, wao hukaidi kabisa isitoshe , wengine hutumia vifaa hivi kuitazama picha zisizofaa mitandaoni. Badala ya kufanya hivyo , wanashauriwa kutumia mitandao hiyo kwa shughuli za kimasomo. Wazazi nao wawaonye watoto wao dhidi ya utovu wa nidhamu.

Hata hivyo simu hizi huchukiza wakati mwingine. Hebu tuchukulie mfano wa mwenyekiti ambaye alikuwa akiongoza mkutano Kisha akapokea simu. Labda alikuwa akingojea simu hiyo na alifikiria kwamba angepigiwa kabla ya mkutano Kwanza. Huenda ikiwa simu yenyewe ni ya dharura , kwa hivyo hatakuwa na jingine ila kupokea simu hiyo. Je, na hao waliokuwa mkutanoni wafanye Nini?Ukweli ni kuwa wataachwa katika Hali ya taharuki huku wakikosa Cha kusema.

Katika visa vingi wakenya wamepoteza pesa zao kupitia simutamba. Kupita mfumo wa “Mpesa” watu hutumia na kupokea hela nyingi mno . Wafanyibiashara wamelalamika sana. Ikiwa ni duka la kuuza bidhaa kama vitabu viatu na hata runinga. Baada ya mtu kulipa pesa, yeye hutumia nambari “456” kudai kuwa ametuma pesa kwa nambari ambayo haistahili . Kisha ” Safaricom” watarudisha hela hizo. Matapeli wametumia njia hii kuwaibia wakenya . Imebidi Safaricom kuhimiza wateja wake kutumia “Till number” kuepuka kunaswa katika mtego huu .

Simutamba hasa ” Safaricom ” huwauzia wateja wake data katika mtandao kwa Bei ghali mno. Si ajabu wengi wamehamia mtandao wa ” Telecom” kwasababu data zake ni Bora mno. Heko kwa mtandao wa ” Telecom” kwa kazi Bora ya mawasiliano.
Hebu fikiria Maisha ya mashambani mahali ambapo umeme haipo . Je, simu yako ikiisha moto, je utafanya Nini, bila shaka itakuwa tatizo ya simutamba. Ikiwa Kuna mgonjwa anahitaji matababu ya dharura , bila shaka kama hakuna “Solar” kutaibuka Hali ya sintofahamu na huenda mgonjwa atafariki akikosa matibabu.

Nchi mbalimbali zimeanza kubuni Sheria za kuzingatiwa katika matumizi ya rununu. Kuna sehemu mbalimabali ambazo mtu anahitajika azime simu. Kwa mfano hospitalalini , kwenye benki , kanisani na hata vituo vya mafuta ya petroli . Ingawa Kuna mabaya yanayoletwa na matumizi ya simutamba, zimefanya tupige hatua katika sekta mbalimbali . Ni bora wakenya kuelewa simu tamba vyema ili wasipoteze hela zaidi.Heko kwa waziri wa habari bwana Eliud Owalo kutia fora katika sekta ya mawasiliano, na kupunguza utapeli wa mtandao.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img