8 C
London
Monday, December 9, 2024
HomeBusinessTechnologyULIMWENGU WA TARAKILISHI NCHINI

ULIMWENGU WA TARAKILISHI NCHINI

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Telenolojia ni maarifa ya kisayanasi yaliyowekwa katika matumizi ya mitambo kama vile viwandani, kilimo , ufundi au mawasiliano.
Vyombo vya kisasa katika njanya hizi zote zinatumia teknolojia. Vyombo hivi husaidia kurahisisha kazi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika ofisini au nyanjani. Ifuatayo ni mkusanyiko wa baadhi ya vyombo vya teknolojia ni runinga , rununu , redio na kadhalika.

Kompyuta ni mashine ya elektroniki ya kuhifadhi na kuchanganua taarifa zilizoingizwa , kukokotoa na kuongoza mitambo. Je, unafahamu umuhimu wa tarakilishi? Kuna baadhi ya watu hutumia kompyuta kwa shughuli mbalimbali, mbona watumia tarakilishi kila mara , ifuatayo ni umuhimu wa tarakilishi nchini kenya.
Tarakilishi pia imeimarika kwani Kuna ndogo ziitwazo vipakatilishi ambazo hubebwa kila mara . Si lazima uandike barua kuipekeka kwenye posta . Unaweza kuandika baruameme au ukawasiliana na mwenzako kupitia ujumbe mfupi kwenye rununu uitwao arafa.

Si kila mgeni anayeingia au kutoka nchini kenya ni rafiki. Ni Bora serikali kuwa makini zaidi.Tarakilishi ni chombo ambacho hutumiwa kuhifadhi habari za siri . Kwa maelezo kuhusu cheti za kuzaliwa na hata vitambulisho huhifadhiwa kwevye tarakilishi. Hii ni njia moja ya kuepuka hatari kwenye uhalifu wa mitandao.
Hapo zamani za kale , ilikuwa aibu sana kutembea mwendo mrefu ili kupitisha ujumbe. Ikiwa mtu amefariki hakuwa na rununu Wala tarakilishi, hata hivyo ikiwa mtu anataka kupiga chapa makala yaani ” photocopy” pia tarakilishi imefanya kazi hii kuwa rahisi sana . Heko kwa teknolojia ya kisasa nchini.
Nchini Kenya Kuna wanahabari wengi sana. Wanahabari Hawa hufanya kazi katika kituo mbalimbali kama “citizen , televisheni arobaini na saba . Ni wazi kuwa wao hutumia tarakilishi katika kazi zao za kila siku. Kuna wale ambao wanahariri habari yaani ” editor’s ” wao kila mara hutumia tarakilishi kuandaa habari zao kwenye mtandao . Kwa hivyo tarakilishi ni chombo chenye manufaa zaidi.

Si ajabu kuwa sisi kila mara huenda kwenye benki . Wakati unataka kutoa pesa kwenye akaunti yako. Yule mhudumu wa benki anatumia tarakilishi ili kuweka data au taarifa zako kwenye mtandao. Bila tarakilishi angechukuwa muda mwingi ili kihudumia wateja wake. Tarakilishi hurahisishi kazi ambayo ingechukua wakati kukamilika. Si kila binadamu ni gwiji wa kufanya hesabu . Kuna wale ambao hesabu iliwapiga chenga wakiwa shuleni. Baadhi ya hesabu ngumu huweza kufanyiwa kwenye tarakilishi. Unapofanya hivyo jawabu hupatikana kwa urahisi.

Mbona uteseke na kuwa na mawazo tele? Si kila binadamu ni mkamilifu . Kuna baadhi ya maneno ambayo si rahisi kujua maana moja kwa moja . Ikiwa mwanafunzi au mwalimu atapata shida kutambua neno au matumizi yake darasani . Basi anaweza kutumia tarakilishi kutafuta maana na matumizi haraka . Jambo hili huwafanya wanafunzi kupenda kutumia teknolojia.
Mtihani unapofanywa ni Bora kujua matokeo kwa haraka kwasababu wazazi Wana haki ya kupinga na kutambua vile mtoto anavyotia bidii.mwalimu anaweza kutumia tarakilishi kuchora maumbo mbalimbali kama vile duara , mstatili na hata mraba. Katika la hesabu unaweza kutumia tarakilishi kuchora grafu za matokeo. Picha nyingi hupatikana kwenye tarakilishi Kama picha za matunda, mavazi, Sara za shule. Hizi zote hurahisishi mtaala wa umilisi yaani “C.B. C ” katika mtaala wa elimu, Kule hospitalini , daktari hutumia tarakilishi ili kujua aina mbalimbali ya dawa . mgonjwa anapofika kwenye zahanati , siku hizi madaktari wengi Huwa wanatumia tarakilishi. Badala ya kupiga foleni kwenye mlango ,basi ujumbe wako hutumwa kwa tarakilishi. Na baada ya muda mchache unapatiwa majibu yako.

Wanabiashara hutumia wavuti ili wapate ujumbe kwa urahisi. Wavuti ni mtandao kwenye tarakilishi ambazo humwezesha mtumizi kupokea ujumbe wowote unaohitajika . Pia anaweza kuchagua bidhaa ambazo anataka kununua kwa kutumia simutamba. Watu wengi pia hawafahamu kuwa wavuti pia huitwa utandawazi. Wale wanabiashara wa kuuza bidhaa barabarani wanaweza kutumia tarakilishi kupiga picha na kutumia wateja wao. Kisha watapeleka bidhaa zao sokoni na kupata riziki tele.
Tarakilishi Huwa ni sehemu muhimu zaidi ambapo ni kioo hasa kinachokuwa mbele au kwenye uso wa runinga, tarakilishi au rununu . Sehemu hii inaitwa kiwambo. Bila kioo basi itakuwa vigumu kutazama picha kwenye kompyuta zetu.

Ukitaka kujua kuhusu taarifa za kampuni kwa ujumla. Bila shaka utatumia tovuti. Ni Bora kufahamu tovuti ni mahali katika tarakilishi iliyounganishwa kwenye mtandao ambapo Huwa na maelezo yanayohusu shirika au kampuni na mtu akitazama hapo anaweza kupata taarifa mbalimbali.
Heko kwa katibu wa mawasiliano ” Eliud Owalo kwa kuroresha teknolojia kote nchini kenya. Vijana wanaweza kuuza bidhaa zao na hata huko shuleni mawasiliano imekuwa rahisi mno.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img