14.8 C
London
Wednesday, October 16, 2024
HomeCommunityHofu Yatanda Kufuatia Mlipuko Wa Mpox

Hofu Yatanda Kufuatia Mlipuko Wa Mpox

Date:

Related stories

African Peacebuilding Network: Individual Research Fellowships

The APN and Next Gen program of the Social...

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open

Applications for IOC Young Leaders Programme 2025-2028 now open Young...

Turmoil in Kenyan Politics; National Assembly Votes to Impeach Deputy President.

In a stunning development that has sent shockwaves through...

How Can African Women Bridge the Digital Gender Gap?

By Guest Writer There is a harsh reality in digital development:...

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya “Monkey Pox” , virusi hivi hutoka katika familia ya virusi vya smallpox. Awali maambukizi yalianza kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu, hasa katika nchi zilizo karibu na misitu ya mvua kitropiki, Mpox kwa mara ya kwanza iligunduliwa kwa miaka ya elfu moja mia kenda sabini kutoka eneo ambalo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ugonjwa huu uligunduliwa kwa kupitia kwa nyani na kutambulika kama homa ya nyani. Maambukizi husambaza kama homa, maumivu ya misuli na mapele makubwa kwenye ngozi, chanjo ya virusi hivyo inapatikana, yenye uwezo wa kudhibiti aina fulani tu ya virusi. Mpox si tishio tu Afrika, ni tishio la kimataifa, tishio ambalo halijui mpaka, halijui rangi wala imani, tofauti na dalili ya vipele kwa kawaida inahusishwa na virusi vya Mpox baadhi ya watu nchini DRC walionyesha makovu tu kwenye viungo vya uzazi.

Watu walio na wapenzi au wapendwa katika mapenzi, wanakabiliana na hatari kubwa ya kuambukizwa gonjwa hili. Nchini Kenya dalili za Mpox zilitokea katika kaunti ya Taita Taveta, kiambu, Kisii, ingawa wagonjwa hawa hawakuwa na virusi hivi. Waziri wa afya mheshimiwa Debra Mlongo Baraza alithibitishia wakenya kauli hii.

Ingwa wakenya wamehimizwa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari kabla ya hatari. Katika maeneo mengi maambukizi na vifo kutokana na Ugonjwa huu kila mwaka huambukiza watoto chini ya umri wa miaka kumi na tano mtawalia. Virusi vya aina ya pili na hatari zaidi, vipo zaidi katika eneo la Afrika ya kati. Na ndio virusi vilivyogunduliwa nchini DRC congo na kuenea hadi nchi ya Kenya, Rwanda, na Uganda. Dalili za Mpox huenezwa kwa mgusano wa moja kwa moja na watu ambao walioambukizwa.

Dalili hii ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe wa mgongo na misuli kuumwa. Maambukizi kwa kawaida huishi na kudumu kati ya siku kumi na nne na hadi ishirini na moja. Kesi mbaya zinaweza kusababisha vidonda kushambuliia kwa mwili mzima, na haswa mdomo, macho na sehemu mbalimbali, baadaye unaanza kuwa na maumivu na inabadilika katika hatua tofauti kabla kutengeneza vipele ambazo hupasuka na kusababisha makovu mwilini.

Mara baada ya kupata homa, upele inaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso Kisha kuenea katika sehemu zingine za mwili, vijanja vya mkono na pia miguu. Hali mbaya zaidi ya Mlipuko wa kimataifa ya Mpox iliripotiwa mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili, ambao ulikuwa umeenea karibu nchi mia moja ambazo hazina historia ya virusi hivi. Shirika la afya ulimwenguni linashauri ikiwa umeambukizwa Mpox unapaswa kujitenga kwa kipindi chote cha maambukizi hadi upele utakapo pasuka.

Pia kufunika vidonda na kuvaa barakoa kunaweza kusaidia kuzuia kuenea. Njia kuu ya kuenea kwa maambukizi ni kugusisha moja kwa moja, mwili na vidonda kwenye ngozi ya aliyeambukizwa, hii inaweza kutokea, lakini ni vyema kuwa waangalifu sana. Kwa mfano kugusana na mtoto wako, ingawa virusi vya Mpox vimepatikana ni vya manii, haijulikani kwa sasa ikiwa vinaweza kusambazwa kupitia majimaji ya ya manii au ukeni, Shirika la W.H.O. linafafanua kauli hii kwa uwazi.

Aidha unashauriwa kujiepusha na kujamiana kwenye vituo kama vilabu, sehemu za kujivinjari na kunyoosha viungo, ikiwemo kujiepusha kutumia pombe na mihadarati katika mazingira mbalimbali.

Mtu yeyote aliye na vipele vipya visivyo vya kawaida anastahili kujiepusha na mapenzi au kugusana kwa karibu na watu wengine hadi atakapofanyiwa vipimo kuhusu maradhi ya zinaa na Mpox mtawalia. Vipimo hivi vitasaidia kuthibitisha hali yako ya afya. Kwa kila visa kumi vilivyoripotiwa kuhusu Mpox tisa vinajumuisha wanaume, idadi kubwa ikiwa bado haijulikani. Gonjwa hili limetipitiwa miongoni mwa wanaume wenye umri wa miaka kati ya ishirini na tisa hadi arobaini inaashiria kuthibitishwa na shirika la dunia.

Shirika la afya duniani limeutangaza ugonjwa wa Mpox kuwa wa dharura kwa afya ya umma ambayo imeibua mashaka duniani. Waziri wa afya Debra Mlongo Baraza alisema serikali imeweka hatua mbalimbali za kukabiliana na Ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuongeza uangalizi, kutoa ushauri kwa wahudumu wa afya kwa lengo la kuwahamasisha juu ya ugonjwa wa Mpox. Kuelimisha umma na kutoa tahadhari kuhusiana na ugonjwa huu miongoni mwa hatua zingine.

Mkurugenzi wa afya ya umma wa kaunti ya Mombasa daktari Salama Swaleh, alitoa ufafanuzi zaidi kuhusu dalili za mpox. Ni Bora serikali kutoa mafunzo ili kuimarisha utoaji wa afya na kuhakikisha jamii zimetahadharishwa kuhusu afya bora. Bi mercy ni katibu wa afya. Katibu mkuu pia alisisitiza kuongezeka kwa uchunguzi na upimaji katika sehemu za kuingilia, ikiwa ni pamoja uwezo mkubwa wa rasilimali. Ni matumani yangu kuwa serikali itapambana na gonjwa hili ili kuokoa maisha ya wakenya, Kama tujuavyo afya ni bora kuliko mali.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img