8.9 C
London
Monday, October 14, 2024
HomeEducationSABABU ZA WANAFUNZI KUGOMA NCHINI KENYA

SABABU ZA WANAFUNZI KUGOMA NCHINI KENYA

Date:

Related stories

Turmoil in Kenyan Politics; National Assembly Votes to Impeach Deputy President.

In a stunning development that has sent shockwaves through...

How Can African Women Bridge the Digital Gender Gap?

By Guest Writer There is a harsh reality in digital development:...

Man, 47, jailed for FGM in Nottingham

The UK is making strides in sending perpetrators of...

Vumbi Ni Hatari Katika Afya yetu?

Vumbi ni hali ya chembe zinazopeperuka hewani za asili...

Fahamu Zaidi Alama Za Barabarani

Alamu za barabarani huweza kuwa nguzo muhumu kwenye kando...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Mgomo ni kukataa kufanya kazi mpaka masharti Fulani yatimizwe au kukataa kuendelea kufanya jambo. Mgomo hufanyika katika sekta mbalimbali kama vile shuleni, mahakamani na hata wananiashara pia hugoma kwasababu mbalimbali.
Sababu za wanafunzi kugoma nchini kenya ni kama ifuatavyo, ongezeko la karo . Wanafunzi wa chuo kikuu Cha Kenyatta walizua malalamishi kuhusu ongezeko la karo . Vyuo vingi hapa nchini kenya zimeongeza karo yake kutokana na Hali ya kiuchumi inayoshuhudiwa humu nchini . Jambo hili limewakasirisha wanafunzi wengi , Kisha wakaamua kupitisha malalamishi Yao kwa migomo.

Kwa kuwa “viboko” vilitolewa shuleni, Ipo idhana miongoni mwa wanajamii kuwa ndicho chanzo Cha migomo ya wanafunzi ya wanafunzi wa shule za upili nchini. Dhana hii. Uzani wake si mzito kwani , jukumu la wazazi Huwa kuwaelekeza watoto wao wakiwa nyumbani.
Malalamishi kuhusu saa za burudani huchangia mgomo. Wanafunzi walilalamika kuhusu mabadiliko ya saa za burudani kutoka usiku hadi mchana. Suala la burudani , halikuwa suala gumu kutatuliwa , ila ulegevu wa utawala wa shule , walimu wangalivalia njuga suala hili bila shaka , uharibifu huo wa Mali ya shule usingalitokea.

Matumizi ya dawa za kulenya . Pia yamekuwa mchango wa mgomo ya wanafunzi shuleni. Dawa ni kitu anachopewa mgonjwa. Mfano wa dawa za kulenya ni kama Bangi katika shule ya upili ya khasoko boys na st Luke boys kimilili zikiwa gatuzi la bungoma, walimu wengi waharakisha kumaliza silabasi hivyo hawawapi wanafunzi fursa nzuri ya kuchangamka kutokana na ukosefu wa wakati nzuri ya burudani, wanafunzi Hawa waliamua kugoma.
Ziara za kitaaalum. Ni jambo la kawaida wanafunzi kizuru sehemu mbalimbali za nchi. Walimu huwahimiza wanafunzi kuchanga pesa za ziara. Hata hivyo vyuo vingi hapa nchini vimekuwa vikiwadai wanafunzi hela za ziara hizi baadaye kuelekea kukamilisha chuo bila Safiri zenyewe kutimizwa.
Mfano Bora ni chuo kikuu Cha pwani kujipata katika Hali ya sintofahamu baada ya wanafunzi wa mwaka wa nne kudai hela zao za Safiri ya kilimo baada ya kunyimwa ilisababisha mgomo wa wanafunzi.

Ufisadi ni Hali ya uharibifu au unyakuzi wa Mali ya umma. Vyuo vingi humu nchini vimewanyima wanafunzi wake ripoti kamili ya utumizi wa fedha humo ndani . Mfano Bora ni chuo kikuu Cha maasai mara ,ambapo bado wanafunzi hawajapewa ripoti kamili kuhusu utumizi wa hela humo chuoni . Jambo hili limesababisha kutoelewana baina ya shule na wanafunzi.
Ukosefu wa rasilimali shuleni au chuoni . Rasilimali ni jumla ya Mali aliyonayo mtu au nchi. Wanafunzi hufurahia masomo wakiwa na rasilimali Bora chuo kama viti vya kukalia. Ni jambo la kushangaza mno. Vyuo vingi humu nchini havina rasilimali za kutosha zitakazowezesha kuendeleza baadhi ya kozi vyema. Wanafunzi wengi walilazimika kurejelea nyumbani baada ya kukosa viti vya kukalia madarasani.

Chuo kikuu Cha pwani kililalama kuhusu ukosefu wa viti ndani ya madarasa.
Ukosefu wa alama za mitihani, Raha ya mwanafunzi ni kupata alama zake baada ya mtihani. Ukosefu wa alama huleta utata na hatimaye migomo ya mara kwa mara.
Hata hivyo wanafunzi wengi wamejipata katika jinamizi la ukosefu wa alama na hivyo kupelekea wengi wao kukosa kuhitimu Vyuo vikuu kwa wakati unaofaa. Jambo hili limechangiwa na mambo huku wahadhiri wa vyuo hivi wakiwa chanzo Cha masaibu haya. Shule mbalimbali pia zimekuwa na matatizo mengi ambayo yamepelekea wanafunzi wengi kukosa alama. Walimu wakuu kwa wakati mwingine hukosa kuwasajili wanafunzi mapema, hatimaye wanakosa kufanya mtihani wa kitaifa.bila shaka wazazi wanaamua kuandaa mgomo.

Wanafunzi kutojiandaa vyema katika mtihani wa kitaifa, hatimaye huchangia mgomo. Kulingana na utafiti ilibainika wazi, kwamba wengi wa wanafunzi hasa watahiniwa, hawakuwa wamejiandaa vyema kukabiliana na mtihani wa kitaifa.(K.c.s.e) na mianya ya wizi wa mitihani iliyokuwepo awali 2015 kurudi nyuma ilikuwa imezibwa.


Wanafunzi ni wanadamu si wanyama. Adhabu Kali isitumiwe kwa wanafunzi shuleni baada ya kukosa. Tendo la matumizi ya” burnsen burner tube”kama kiboko Cha kuwaadhibu Wanafunzi shuleni yafaa kufika mwisho.
Kwa walimu, walimu wasitumie ujio wa korona kuwa chanzo Cha utovu wa nidhamu shuleni ila, wajifunze kuwasikiliza wanafunzi wao ili kupunguza mgomo shuleni.Tusisahau pia chakula kibaya au mbovu husababisha mgomo maendeleo ya shule. Ni Bora kuhusisha wazazi kwa maendeleo ya shule. Wizara ya elimu kutoa njia mbadala kusuluhisha matatizo ya wanafunzi. Wakifanya hivyo basi migomo ya wanafunzi itapungua.

Kule Gatuzi la Uasi Ngishu , katika shule ya upili ya mafuta, wazazi walimfurusha mwalimu mkuu, kwasababu ya matokeo duni, jambo hili lilimfanya katibu wa elimu Nancy macharia kuwaondoa walimu walioajiriwa na “TSC” wale ambao waliumia ni wanafunzi, kwasababu walikosa masomo.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img