6.8 C
London
Wednesday, December 11, 2024
HomeHealthUmuhimu Wa Kudumisha Afya Bora

Umuhimu Wa Kudumisha Afya Bora

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Afya ni bora zaidi kuliko Mali. Ni jukumu la kila mwananchi kudumisha afya bora. Afya hujumuisha kupiga mswaki , kuoga na hata kifua nguo. Ukosefu wa afya bora husababisha maradhi. Je, ni muhimu kupiga mswaki kila siku mara tatu au mbili kwa siku? Wakati mtu anapozungumza mbele ya hadhira, ni vyema awe na hewa safi kutoka kinywani, Kuna baadhi ya watu ambao hawapendi kupiga mswaki.

Kuna mambo kadha ambayo husababisha kutoa harufu mbaya kinywani. Si vyema kuvuta sigara, bali na harufu mbaya, sigara hukausha kunywa chako na kusababisha mazalio ya bakteria, Hali hii humfanya mtu kuwa na harufu mbaya kinywani wakati unapozumngumza mbele ya watu.
Kuna baadhi ya watu ambao hunywa pombe bila kufahamu kuwa pombe Ina madhara kinywani, pombe hukausha kunywa, Kisha mazalio ya bakteria ndani ya kinywa chako husababisha harafu.

Tatizo la kunuka mdomo huwakera watu wengi sana, hata baada ya kupiga mswaki, bado wananuka mdomo. Utasikia marafiki zao wanazungumza vibaya kukuhusu hata wengine hukutoroka. Hali hii husababisha upweke. Si ajabu kuona watu wengi hununua ” chewing gum” ili wanukie vizuri kunywa.

Lakini tatizo hili la kunuka mdomo imekuwa sugu zaidi.Wakati mtu anatoa harufu mbaya mdomo itamfanya ashindwe kujiamini wakati anazungumza na watu. Pia watu wengine wanaweza kukushuku kuwa wewe ni mchafu , bali hawajafahamu kuwa ni maradhi.Utafiti wa wanasayansi ni kwamba, ni vigumu sana kufahamu kuwa una harufu mbaya, lakini ni rahisi sana kutambua harufu kutokana kwa kinywa cha mtu mwingine.Unaweza kujua harufu mbaya kinywani, kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa , hata wengine hupumua mbele ya kioo Kisha unanusa,

Wanapofanya haya yote ni rahisi kutambua kinywa chako kinatoa harufu mbaya. Vilevile unaweza kutumia kijiti Cha kuchokonolea meno na kukinusa, utagundua harufu ipi inatoka katika kinywa chako, Namna bora zaidi ya kuzuia kinywa kutoa harufu mbaya ni kupiga mswaki mara mbili kwa siku asubuhi na jioni na kufanya flosi mara moja kwa siku .

Ikiwa una wakati wakutosha muone daktari wa kinywa na meno mara kwa mara baada ya miezi sita . Kuoza kwa meno huwa na hatari sana, dalili zinaweza kujumuisha maumivu kisha ugumu wa kula chakula.Kaviti inaweza kuwa na aina tofauti za rangi kubadilika kutoka kijani kibichi hadi nyeusi .

Matatizo ya meno hufanya mtu kupoteza jino na maambukizi au usaha hutokea, mtu anaweza kuwa na hamu ya chakula, lakini kwasababu ya changamoto hizi hawezi kula chakula kwa amani. Ili kuboresha afya ya kunywa chako, inafaa ubadilishe mswaki wako baada ya miezi tatu au nne.

Usingojee mpaka mswaki wako uharibike, pia ni bora kutumia dawa yenye madini ya fluoride. Kupiga mswaki kila siku huondoa taka au mabaki ya vyakula, jambo hili husaidia kuondoa bakteria mdomoni.Bakteria ikirundikana mdomoni hufanya meno kuoza hatimaye kusababisha magonjwa ya ufizi. Fluoride husaidia kupunguza utando, ni bora kuitumia ikiwa tayari una ufizi unaovuja damu badala ya kipimo cha kuzuia.

Isitoshe wengi wanasema kuwa kupiga mswaki kabla ya kufungua kinywa ni bora, kiliko kupiga mswaki baada ya chakula.Ilhali madaktari wa meno wanapendekeza kupiga mswaki baada ya chakula, kwani hali hii huondoa sio tu utando bali pia mabaki ya chakula mdomoni mwako.

Kupiga mswaki vizuri huweka meno na ufizi katika afya nzuri na hupunguza hatari ya kupata ugonjwa sugu, lakini ni watu wachache ndio wanajua jinsi ya kupiga meno mswaki.Wakati mtu anapiga mswaki, si vyema kutumia nguvu kupita kiasi , hali hii inaweza kuharibu ufizi wako .Majeraha katika tishu laini yanasababishwa na kupiga mswaki kupita kiasi hutoa njia ya kuingia kwa bakteria kwenye mkondo wa damu. Kupiga mswaki katikati ya meno au kutumia dawa za kuosha kinywa ni bora ikiwa una Ugonjwa wa ufizi ingawa, unaudhi lakini inafaa kufanya hivyo.

Kupiga mswaki hupunguza hatari ya harufu mbaya kinywani pamoja na kubadilisha rangi kwa meno na matundu.Watu wengi bado wako gizani , hawajafahamu kuwa kupiga mswaki hupunguza hatari ya Ugonjwa wa kisukari ya aina ya pili , Ugonjwa wa moyo na mishipa.

Usafi wa kinywa hupunguza Ugonjwa wa ufizi.Fizi hujivuta kutoka kwenye meno na hivyo hufanya meno kuonekana ni mrefu kuliko ya kawaida.Meno huachana na kutengeneza nafasi mpya katika meno yako ambazo hazikuwepo awali. Kuna aina mbalimabali ya dawa ya meno ambazo hutumiwa kupiga mswaki kama vile close-up, Colgate, na zinginenezo. Bakteria na vijududu wanaoishi katika kinywa cha kila mtu huunda “biofilm”. Utando nyembamba ulio na bakteria unayoitwa “plaque” ni eneo muhimu ya kuondoa plaque kwenye mstari wa ufizi wa meno.

Wakati wa kupiga meno mswaki, ni bora zaidi kuwa mwangalifu, tusisahau kupiga ulimi mswaki.Dawa ya meno yenye uwezo wa kungarisha na kusugua sehemu ngumu huitwa “whitening”meno yanapoendelea kuchakaa huwa na kidonda au matundu kadhaa.Ni bora kubadilisha mswaki wako kabla hujaanza kugawanyika.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img