14.9 C
London
Sunday, November 24, 2024
HomeBusinessTechnologyTeknolojia Ya Roboti

Teknolojia Ya Roboti

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Roboti ni mashine hasa inayoweza kuratibiwa na kompyuta yenye uwezo wa kutekeleza mfululizo tata wa vitendo vya kiotomatiki. Nilipokuwa jijini Nairobi maeneo ya kilimani, nilishangaa kuona roboti katika mkahawa mmoja, baada ya kuagiza chakula niliona roboti akibeba mlo taratibu hadi katika meza ya wateja.

Pia ukiwa na siku yako ya kuzaliwa baada ya kulipa pesa, roboti huyu angeweza kukuimbia, ni rasmi kuwa ukitembelea maeneo ya Kilimani hutakosa mkahawa huu. Roboti inaweza kuongozwa na kifaa cha kudhibiti nje, au kudhibiti malengo yake makuu, na huongozwa na zinaweza kutengenezwa ili kuamsha umbo la binadamu, lakini robiti ni machine zinazotekeleza kazi, iliyoundwa kwa msisitizo wa utendakazi mkali, badala urembo unaonekana, huenda binadamu wakapoteza nafasi zao za kazi kutokana na ukuaji wa akili bandia. Kuna robiti za viwandani. Roboti zinazoendesha matibabu, robiti za kusaidia wagonjwa.

Roboti huiga mwonekano unaofanana na maisha au mienendo ya kiotomatiki, roboti inaweza kuwasilisha hisia ya akili au mawazo yake mwenyewe. Mambo ya kujitegemea yanatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo huko roboti za nyumbani na gari linaloendeshwa kwa teknolijia. Tawi la teknolojia linalohusisha muundo, ujenzi, pamoja na kompyuta kwa udhabiti, maoni ya hisia. Teknolojia ya roboti hizi zinahusisha mashine zinazoweza kuchukua nasafi ya wanadamu kwa sura, tabia au uvumbuzi. Roboti nyingi leo zimechochewa na maumbile yanayochangia uga wa roboti zimeundwa tawi jipya zaidi la roboti.

Ili kundi la roboti lifanye kazi kwa pamoja watafiti lazima waanzishe mwilingiliano wao kwa kutege vijenzi vya hali ya juu. Ikiwa roboti ni rahisi na ukosefu wa programu ya hali ya juu, tabia iliyoratibiwa inaweza kupatikana mara chache. Watafiti waliripoti kuwa waliweza kuondoa vitambuzi vyote, mawasiliano, kumbukumbu za hesabu kutoka kwa roboti na waliotumia sifa zawili za roboti kukamilisha seti ya kazi kulingana na tabia. Uigizaji wa roboti husaidia kusoma vipengele mbalimabali vya mfumo ambayo havikuweza kuangaliwa katika maabara.

Pamoja na maendeleo ya haraka ya akili ya bandia na teknolojia ya robotiki, mstari ya uzalishaji wa kiotomatiki inazidi kuwa ya kawaida kati yao yaani “polishing robots”, kama roboti muhimu ya viwandani hutumiwa sana katika tasnia mbalimbali kama vile vitambuzi vya kuona, vitambulisho vya mbali na vitambuzi ambazo hutumia nguvu ili kutambua usahihi na kukabiliana na kazi katika wakati wa mchakato wa kuhakikisha ufanisi bora.

Baadhi ya umuhimu wa roboti na kupunguza gharama za uzalishaji, kukuza ushiriki bora wa habari kati ya wazalishaji, kuboresha ugavi, kupunguza ubadhirifu wa chakula na kuongeza uzalishaji na kuimarisha uendelevu wa kifedha. Katika sekta ya usafiri wa reli, roboti za kung’arisha vyema uso wa miili ya magari ili kuboresha kilimo kwa kuongeza uzalishaji na kujaza pengo la wafanyikazi. Wanaweza kuchukua nafasi ya watu ili kukamilisha kazi zenye kuchosha na zinazojirudia kwa kujitegemea na zinaweza kuwafanya wakulima kuzingatia zaidi usimamizi, roboti ni ya faida ili kuhakikisha zinaunganishwa ili ziwe akili, Tanzania imepiga hatua zaidi kwenye masuala ya teknolojia kiasi cha kutumia roboti almaarufu “Eunice” mwenye uwezo wa kuongea na aliweza kuwakaribisha wageni waliokuwa bungeni.

Muda mfupi baadaye picha na video za roboti Eunice zimegeuka kuwa gumzo mkubwa kwenye mtandao wa kijamii. Katika baadhi ya video za kushangaza zilizonaswa kutoka kwa roboti aliingia ukumbini mwa bunge akitangamana na wabunge ambao pia walipa nafasi ya kusimia na kuuliza maswali na roboti huyo Kisha akajibu. Teknolojia ya roboti inakuza mapinduzi katika nyanja ya kilimo, hapo awali makampuni makubwa yalikuwa tayari kutumia sayansi na teknolijia ilirahisisha kazi zoa.
Teknolojia bunifu kama vile vivinaji vinavyotegemea mashine za kukamua zinazosaidiwa na roboti bila shaka hoboresha ufanisi wa kazi.

Hata hivyo mashine hizi bado zinahitaji uendeshaji wa mwongozo. Ndoto ya wasichana wa shule ya ya upili ya Mbaikini huko Mwala kaunti ya Machokos katika mashindano ya kimataifa ya utumizi wa roboti, ingali mpangoni. Licha ya kukosa pesa za kugharamia safari. Wanafunzi hao watatu wastahili kusafiri hadi Uturuki kwa mashindano hayo mwezi wa Novemba. Roboti katika elimu ni fani inayokua ambapo roboti hufunza wanafunzi masomo huku zikishirikiana nao kupitia vipengele vya uso vinavyofanana na binadamu na teknolojia ya utambuzi wa hisia.

Ili kuunda roboti zenye uwezo mkubwa zinazoweza kubadilika, ni muhumu kutumia data kutoka kwa nyenzo anuwai. Data ya mtandao, data ya uigaji wa data ya mtandao, roboti hutoa maarifa na manufaa ya kipekee kwa mafunzo ya roboti. Kuchanganya aina hizi tofauti ya data kwa ufanisi itakuwa Jambo muhimu katika mafanikio ya utafiti na maendeleo. Pia shule ya upili ya Mangu kupitia teknolojia iliunda roboti, si vyema kwa watu kuwa na wasiwasi kuwa roboti itafanya wapoteze kazi, roboti ilizinduliwa ili kurahisishia binadamu kazi kwa Nia ya kuokoa muda wao.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img