3.1 C
London
Wednesday, January 22, 2025
HomeInternationalKENYAFaida za Ugatuzi na Harasa zake Nchini Kenya(Swahili)

Faida za Ugatuzi na Harasa zake Nchini Kenya(Swahili)

Date:

Related stories

Why Emotional Literacy Matters for Children

Building a Strong Foundation: Why Emotional Literacy is Essential...

Mind Management, not Time Management.

The Illusion of More Time: Why Mind Management Trumps...

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Ugatuzi Ni mfumo wa serikali ambao karibu unafanana na majimbo. Ni mfumo wa kugawanya madaraka na ugavi wa matumizi ya rasilimali katika serikali kuu.
Lengo kuu ya ugatuzi Ni kuonyesha uwezo katika Shughuli za kazi mbalimbali. Mfumu wa ugatuzi ulianzishwa mwaka wa elfu mbili na kumi(2010) . Hapa ndipo Kenya ilijinyakulia katiba mpya. Baada ya katiba kulikuwa na serikali mbili kuu maalum. Hii Ni serkali kuu na serikali za kaunti Tunazo kaunti arobaini na Saba humu nchini.

Matunda ya ugatuzi ni mengi Kama vile ifuatavyo:

Hatua zimepigwa kuleta huduma karibu na mwananchi wa kawaida . Katika gatuzi la kakamega aliyekuwa Gavana Oparanya alijenga soko maalum . Hali hii ilibadilisha maisha ya wafanyikazi mjini kakamega. Pia taa za mulika mwizi ziliwekwa katika soko Hilo ili wafanyibiashara waendeleze Shughuli zao Hadi usiku.

Katika sekta ya elimu shilingi milioni ishirini na moja ilitolewa kujenga bweni katika shule ya kilimo. Haya yote Ni matunda ya ugatuzi katika kaunti ya kakamega. Hapo zamani hudumu zote zilifanywa mjini Nairobi. Ilikuwa vigumu kuhudhuria mkutano kwa haraka na huenda mtu atakosa nauli au kuchelewa kazini. Sasa hivi utaw hata ofisi ya Gavana. Vijana wameweza kupata ajira kwa haraka. Kama vile aliyekuwa rais Kenyatta aliwasajili vijana kwa mradi wa ” kazi kwa vijana”

Katika mji mbalimbali Barabara haijakarabatiwa kulitokea ajali nyingi mno barabarani.usafiri ulikuwa Ni tatizo. Kwa sasa Kuna maendeleo , miundo misingi Imeboreshwa katika gatuzi la kiambu Kuna Thika “superhighway,” hata kule Githurai 45 Kuna Barabara ya wasafiri yaani “superhighway” ambayo huitwa kivukio katika lugha ya kiswahili.

Hudumu zote muhimu zinapatikana humu mjini. Kuna kituo Cha polisi , kituo hiki huwasaidia wakaaji kudumisha usalama wao kijijini. Chifu ndiye husikiliza kesi kule kijijini , kwa hivyo utovu wa usalama umepungua kwa kiasi kikubwa. Ikiwa Kuna hali ya dharura kijijini wananchi huripoti kwa wazee wa Kijiji . Haya yote Ni thibitisho kuwa ugatuzi Ni nguzo kuu kwa wananchi.

Wanawake walikuwa wamebaguliwa katika sekta ya uongozi. Sasa hivi gatuzi la Nakuru imewahusisha wanawake katika uongozi. Kuna Susan kihika ambaye Ni gavana wa Jimbo la Nakuru , kule Meru kuwa gavana kawira mwangaza. Hii Ni thibitisho kuwa jinsia zote zimehusishwa kwenye uongozi. Serikali ya kitaifa pia haijaachwa nyuma kuchagua wanawake. Jaji mkuu Ni mwanamke anayeitwa Martha koome Kama mwanamke ameboresha mahakama zetu huku akijenga mahakama zaidi . Usawa katika uongozi Gatuzi nyingi Zina makabila tofauti tofauti . Katika uteuzi . Si jamii moja tu ndio huongoza. Mikakati imezingatiwa kuona kila kablia imetoa mwakilishi wao . Kitambo Shughuli za uongozi zilifanywa katika serikali kuu . Watu kule mashinani walikosa huduma na kufikia malengo yao kamilifu.

Rasilimali umeweza kutumiwa na wananchi wenyewe . Kuna mbolea ambayo wakulima wamepatiwa na serikali kuu. Wakulima wengi walianda mashamba yao saa hivi wanatarajia kuvuna mazao mengi . Iwapo haingekuwa ugatuzi mbolea hii ingechukuwa muda mrefu kuwafikia wananchi . Heko kwa naibu rais bwana Gachagua kufuatilia Shughuli hii kwa uwazi.

Maabara ya kisasa imejengwa. katika siki hizi za jadi , wananchi waliteseka zaidi. Hivi majuzi Gavana wa Trans Nzoia bwana Natembeya alizindua hospitali mpya ya ” kijana wamalwa Referal” wakaji walifurahia Sana. Huduma muhimu Kama upasuaji utafanyika bila tatizo. Pia ni furaha kwa madaktari ambayo wamepata kazi ya kutoa huduma kwa wagonjwa. Wananchi hawajaachwa nyuma wao pia biashara yao itanoga wakiwauzua wagonjwa bidhaa mbalimbali Kama matunda na maji Safi ya kunywa.

Wananchi wameweza kugundua haki zao za kikatiba . Baada ya kusoma katiba na kuielewa vyema, wao hutoa malalamishi yao ikiwa Barabara haitajengwa vizuri utawaona wanaandamana Hadi kwa ofisi ya Gavana.pia dawa zikikosekana kwenye zahanati bila shaka watalalamika. Ni haki ya kila mwananchi kupata maji Safi, elimu na hata Barabara Bora. Ugatuzi umewasaidia kuboresha miundo misingi ili kuzuia migomo ya kila Mara. Gavana wa Busia Paul otuoma hajaachwa nyuma kukarabati Barabara mbovu kwa juhudi zake zote.

Ingawa wananchi walifurahia ugatuzi , Kuna changamoto zaidi . Baadhi ya wananchi Wana kilio Cha haki . Maisha imekuwa magumu zaidi. Kuna ongezeko la kodi . Serikali imewaongezea Kodi kupita kiasi. Jambo hili limewakera kupita kiasi na kukosa mahitaji yao muhimu.

Tatizo la mshahara kuchelewa imekuwa donda ndugu . Ni kilio kila mwezi . Kituo Cha posta mjini Busia Hadi sasa hawajapokea mshahara wao Hadi sasa hivi. Watoto wao wamekosa kuhudhuria masomo yao . Hii Ni baada ya serikali kukosa kutatua shida yao na kuwalipa haki yao mapema.

Kuna mgawanyiko Kati ya serikali kuu na majimbo. Tatizo katika sekta ya afya Ni kuwa madaktari wanagoma kila Mara. Dawa pia hazipo na wagonjwa hulalamika kugharamika kupita kiasi . Je sekta ya afya inafaa kuendelezwa vipi ? Kuna tofauti ya kimaendeleo katika gatuzi , ukitembelea kaunti ya Mombasa Kuna anga tua nzuri ukilinganishwa na kaunti ya Baringo . Ni Bora tuwe na usawa katika maendeleo . Gatuzi inahitaji mabadiliko kwa kuvutia watali siku zote.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img