5.7 C
London
Sunday, December 22, 2024
HomeEnvironmentKilimo Cha Pamba

Kilimo Cha Pamba

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la pamba. Pamba ni kata ndani ya Jiji la mwanza. Nyuzi za pamba huonekana kama sufi na mipamba inalimwa kwa nyuzi hizi. Pamba inawakilisha bahati kutoa na kuchukua, shukrani , kupokea baraka, thamini na ustawi. Wakulima wa pamba mjini Busia wamenufaika na mbegu. Wizara ya kilimo imetoa tani kumi na saba za mbegu.

katika Nchi yetu, Kuna aina nyingi za mimea inayokuzwa. Mimea hii ni kama mibuni, michai, minazi, mipamba na mingineyo mingi. Mimea hii hukuzwa katika sehemu mbalimbali humu nchini kama vile Busia, Mombasa na hata Siaya. Pamba huwaletea wakulima faida kubwa wanapouza mazao Nchi yetu hupata manufaa ya pesa za kigeni.

Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa humu nchini. Lakini licha ya hivyo watu wengi hawajakumbatia sana ukulima wa mimea huu. Ni wazi kuwa baadhi ya wakulima wanaendeleza ukulima wa Pamba, katika kaunti ya kwale. Bidhaa za viwandani zilizo na pamba ni tofauti kama, vifuriko vya ukuta, viungo vya vitabu na Kanda za zipu. Watumiaji wakubwa wa pamba katika kitengo hiki ni vifaa vya matibabu, nyuzi za viwanda na turubai.

Nyuzi husokotwa kutengeneza Uzi na hufumwa ili kutengeneza vitambaa. Spika wa bunge la kitaifa mheshimiwa Moses wetangula amewahimiza wakulima wa kaunti ya Busia, kurejea kilimo cha pamba. Serikali Ina mpango wa kufufua viwanda vya kutayarisha pamba.

Katika kaunti ya Homa Bay serikali inawania kuimarisha uzalishaji wake katika sekta ya pamba na kilimo Cha samaki na biashara. Gavana wa Homabay Gladys Wanga anawakaribisha waekezaji kutoka pande zote duniani. Pesa za kigeni hutumiwa kununulia bidhaa mbalimbali ambazo hazipatikani huku nchini.

Kutokana na pamba, tunapata vitu tofauti kama mafuta ya kupikia ,nyuzi za kushonea , chakula cha ng’ombe na hata pamba zinatumika hospitali. Lakini baadhi ya kulima kaunti ya kwale, kilimo Cha pamba ya kisasa kimeimarisha maisha yao, kilimo cha pamba kinaendelezwa eneo bunge la Lungalunga na Mzee James Kithio Musyoka. Mzee huyu amefanya kilimo cha pamba kwa zaidi miaka Tano. Kilimo Cha pamba kimeweza kumpatia mapato mengi. Amesomesha watoto wake na kununua ng’ombe wa kufuga. Mimea wa pamba ni bora zaidi kwasababu inastahimili kiangazi hivyo basi ni njia mojawapo ya kufanya ukulima kunawiri licha ya mabadiliko ya tabianchi, yanayoshuhudiwa ulimwengu mzima.

Ukulima wa Pamba umefufuliwa Hola kaunti ya Tana River. Jambo hili litawanufaisha wakazi zaidi. Mamlaka ya unyunyizaji mashamba maji yasema aina pamba ya B.T. inanawiri vyema.Je, pamba hutengenezwaje mpaka ikawa nguo? ikishavunwa shambani hupelekwa viwandani.Humo mna mashine kubwa ambazo huipokea na huifinyafinya katika mashina zingine ambazo huifinyafinya mpaka ikiwa kama blanketi refu la pamba tupu.

Baadhi ya changamoto ambazo wakulima wanapitia katika ukulima wa Pamba ni pamoja na wadudu wanaoingilia majani na wanaoharibu rangi ya pamba wale wanaofyonza maji na kufanya pamba hiyo kukosa wakulima wa pamba katika kaunti ya Kwale.

Katika Kijiji jirani Cha Sagalato wadi ya Kikoneni eneo bunge la Lungalunga kaunti ya kwale. Maulidi Omar anaendeleza shughuli za kuvuna pamba ya kisasa katika ekari moja ya shamba lake.Wetangula alipigia upato kilimo Cha Pamba huku akiwashauriwa wakulima watumia mbegu mpya za zao la pamba ambazo zitahakikisha mazao bora.
Blanketi za pamba hutiwa katika mashine zenye menomeno ambazo huchana nyuzi hizo za blanketi na kuzifanya kuwa namna ya kamba nene kidogo.Kamba hiyo hupitishwa kwenye mashine ambazo huigawanya katika nyuzi za unene mbalimbali, nyuzi zenyewe huwa laini , mbalimbali na vitambaa vyepesi au vizito.

Baada ya kufumwa , vitambaa hivyo hupitishwa katika mitambo ambayo huvifua viwe safi .Kwa vile hatuwezi kuwa na vitambaa vya rangi ya aina moja mbalimbali. Baadaye vile vitambaa hukaushwa na kufungwa katika majora tayari kwa kuuziwa wenye maduka .Kwa hivyo wananchi hununua majora haya na kushona mavazi kama mashati, marinda na suruali.

Serikali ya kenya itawapa wakulima wa pamba mbegu na kuwapiga jeki zaidi. kilimo cha pamba hufanyika Teso kaskazini . kiwanda Cha pamba Malakisi kilizinduliwa miezi mitatu iliyopita .Kuna aina za pamba kama Hart 89 na Ksa 81m Zina uweza wa uzalishaji wa kilo elfu mbili hamsini, Pamba huhitaji kiasi cha mvua 25 mm kwa miezi miwili ya kwanza udongo wenye PH chini ya 5.0 pamba haistawi vizuri .

Wakulima wa pamba Lamu walitaka serikali kuwasaidia ili kuimarisha kilimo Cha pamba . Pamba hutumiwa kutengeneza sodo ambazo hutumiwa na kina dada wakati wa hedhi. Pia hospitalini pamba hutumiwa na daktari wakati wa kudunga sindano, hata pamba hutumika kufungia kidonda .Ni bora wakenya kukuza pamba ili kuboresha maisha yao , kilimo ni uti wa mgongo .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img