krimasi ni siku ambayo mwikozi yesu kristo alizaliwa . Siku hii almaarufu noeli au krimasi husherehekewa tarehe ishirini na Tano mwezi wa kumi na mbili kila mwaka . Wakenya wengi wajianda vyema ili kusherehekea siku hii kwa shangwe na nderemo. Mkesha wa sherehe huanza tarehe ishirini na nne, ambapo wakristo hutengamana katika makanisa mbalimbali katika maombi . Ilikuwa lazima kama ibada wakenya kusafiri maeneo mbalimbali za nchi kuungana na familia zao.

Hata hivyo sherehe hii ilikuwa na changamoto chungu nzima. Katika sehemu za Mombasa wananchi waliathiriwa na mafuriko . Nyumba zao zilijaa maji, hata kinamama walikosa chakula , ilikuwa vigumu kulala Raha mstarehe , walikesha kwa baridi Kali wakitetemeka. Katika hekaheka za kuelekea mashambani. Madereva walikiuka Sheria za barabarani. Kule maeneo ya londiani na kericho , wakenya wengi walipoteza maisha Yao. Sababu kuu ni dereva kupoteza mwekekeo na Kisha kusababisha ajali barabarani . Ni jambo la kushangaza kuwa maisha ya wakenya Hawa ilikatizwa kighafla. Maisha ilibadilika kutoka kwa raha hadi karaha. Majeruhi walipelekwa hospitalini ili wapate matibabu.

Krimasi ya mwaka huu ilikuwa ya ajabu mno. Wazazi wengi walikosa fedha za kuwanunulia watoto wao nguo za sikuku . Tatizo kubwa ilikuwa gharama ya maisha . Wengi wao walikata kauli kununua chakula badala ya nguo . Fehda zote walizitengea karo . Safari nyingi za kusafiri katika mbuga ya maasai mara kule narok ilikuwa ni ndoto tu . Ni heri kuwatazama wanyama Hawa kwenye runinga , kuliko kusafiri . Wazazi wengi walijutia kauli hii kwa mapana na marefu. Bei ya mafuta iliwatia kiwewe madereva , walitarajia Bei ya mafuta itashuka.
Lakini ndoto Yao haikutimia .Hali hii iliwafanya kupandisha nauli maradufu. Wakilaumu serikali kupunguza Bei ya mafuta kwa shilingi Tano tu .
Wakazi wa lamu walipitia masaibu chunu nzima. Hali ya usafiri ilikuwa tatizo. Katika hoteli nyingi kulikuwa na ukosefu wa umeme watalii walipatwa na mshangao. Ukosefu wa umeme , walatii walipatwa na mshangao .ukosefu wa umeme imechukua sasa miezi tano.wakazi wakizidi kulalamikia serikali ya kaunti pamoja na kitaifa . Wale wafanyibiShara walikadiria hasara mno nyama, samaki, ziliharibika kwenye ghogofu.Ni ombi langu serikali itachukulia Jambo hili kwa uzito . Pia kufunga ndoa illikuwa tatizo.