15.8 C
London
Sunday, November 24, 2024
HomeInternationalKENYAJINSI YA KUZUIA UFISADI NCHINI KENYA

JINSI YA KUZUIA UFISADI NCHINI KENYA

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Ufisadi ni matumizi mabaya ya mamlaka ili kujinufaisha kibinafsi. Ufisadi ulianza zamani na imekita mzizi hata sasa. Ufisadi inahusisha mambo mengi , si kula rushwa tu, maafisa wa umma huiba Mali, na hukubali kupokea hongo kwa hudumu ambazo hazistahili.
Hata hivyo nchini kenya viongozi hutumia vibaya vyeo vyao kuwanufaisha marafiki na pia watu wa ukoo . Sehemu ambazo ufisadi imekita mzizi ni katika vyama vya kisiasa , idara ya ulinzi , maafisa wa umma , bungeni na hata mahakamani.

Ufisadi unaweza kutokea katika namna mbalimbali. Hongo inamaanisha kwamba mtu , shirika au taasisi kwa maksudi huchukua au hutoa hongo katika bidhaa bila idhini, kinyume Cha malipo inavyostahili.. ubadhirifu wa hela ni wizi wa rasilimali kwa ajili ya matumizi ya kibinafsi.
Ulaghai ni kosa la jinai la udanganyifu ili kupata faida kwa njia ya kudhulumu . Uporaji ni fedha ambazo zinachukuliwa kwa mtu kwa njia ya nguvu.
Upendeleo ni Hali ya kupenda mtu mmoja au kikundi Cha watu kutokana na kitu Fulani kwa njia ambayo si ya kawaida kwa wote, udugu ni aina ya upendeleo, ambao mmiliki wa ofisi mwenye mamlaka ya uteuzi anapendelea kupendeza wanafamilia wenzake , bila kujali sifa zao.

Nchi fisadi zaidi ni somalia , Syria Sudan kusini , Venezuela ,Korea ya kaskazini, Burundi, na hata Libya na equatorial Guinea.
Ufisadi nchini kenya ni tishio kuu kwa ufanisi wa jamii. Kama vile “E.A.C.C.” hatawezi kuukabili peke yao , Bali tunaongoza tu vita dhidi yake kama taasisi akasema bwana Ngumbi.
si ajabu kufahamu kuwa Rais Ruto alisisitiza kuwa ufisadi umekithiri ndani ya idara ya mahakama , akiahidi kupambana na majaji fisadi wanaohujumu ajenda yake ya mabadiliko nchini kenya. Jambo hili lilimfanya kuandaa mkutano kati yake na Martha koome, ili kuleta utangamano.

E.A.C.C.” yawanasa maafisa Tisa wa K.PA. kwa ulaghai wa zabuni . Watu Tisa wakiwemo maafisa wa halmashauri ya bandari nchini “K.PA.” watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi dhidi Yao kulingana na timu ya maadili.
Kiongozi wa upinzani Raila odinga pia alikashifiwa serikali ya kenya Kwanza akidai kuwa ni fisadi zaidi haswa sekta ya mafuta . Isitoshe pia sukari ghushi ilinaswa kule Mombasa.
Paul Mackenzie anashutumiwa kuwa fisadi kuwadanganya wakristo . Mawakala na mashirika ya haki za binadamu yameelezea masikitiko katika ukiukaji wa Sheria na kusababisha vifo . Wakili Abdullahi Nasir alimwonya rais Ruto kuhusu kuwepo kwa hongo katika mahakama wakati wa kutoa uamuzi.
Katika hospitali za umma bado ufisadi umezidi , dawa hazipo , ilhali serikali Inatoa huduma bila malipo . Hata shuleni ufisadi umekita mzizi . Hiyo ndio maana Rais William Ruto anahimiza karo ya shule zilipwe na mfumo wa ” ecitizen” ilhali wananchi wanapinga maoni hii, walitoa hisia zao mbalimbali, hata hivyo ni Bora kutoa suluhisho ifuatavyo ili kuzuia ufisadi nchini kenya.
Pana haja ya wananchi kubadilisha mtazamo wao kuhusu ajira ya serikali na badala yake wategemee kujiajiri wao wenye kupitia njia ya kubuni ajira.

Serikali inafaa kubuni taasisi maalum kupitia kwa wizara ya fedha ambapo vijana wanaweza kupata mikopo ya kujiendeleza. Vijana Wana ujuzi lakini wanakosa yule maelekezi ili kupata mashauri zaidi . Serikali ilifanya hivyo janga la ufisadi utatupwa katika kaburi la sahau na bila shaka kutakuwa na maendeleo katika kaunti na vijiji vyetu.
Mashirika ya kifedha ni Bora kutoa mikopo ya riba ya chini kwa vijana na wajisiaamali wengine ili waweze kujiendeleza na kujitegemea. Ni Bora pia serikali iondoe vikwazo na urasmi mwingi katika mchakato mzima wa kuanzisha biashara na ajira.

Makongamano na semina maalum ziandaliwe ili wananchi wapate mafunzo kuhusu namna ya kuchagua na kuendeleza biashara.
Vyuo vikuu vitathmini na kuondolea mbali baaadhi ya kozi ambazo hazina umuhimu wowote ikizingatia la soko ajira . Pia vyuo vya kiufundi vijengwe ili kutoa mafunzo kwa vijana wote .
Vituo zaidi vya Talanta vijengwe katika kila gatuzi ili kutoa nafasi au jukwaa kwa vijana kunoa Talanta zao na kujiendeleza. Ufisadi unaoshuhudiwa katika sekta ya ajira umulikwe na wahusuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili wanaostahili ajira wapate kuajiriwa.

Umri mahsusi wa Kustaafu uwekwe na kuzingatiwa ili kuhakikisha kuwa kizazi kichanga pia kinapata ajira, kote nchini na kaunti. Serikali ihakikishe wasomi wote wamepata ajira pindi wanapofuzu kutoka vyuoni. Wanapokamilisha kusomea kozi mbalimbali katika sekta za umma au kibinafsi.
Serikali iwekeze zaidi katika vyuo vya kiufundi ( ujenzi na ununuzi wa vifaa ) muhimu za mafunzo. Pia kufanya ubia na mataifa mengine katika sekta ya ajira ambapo wasomi na wataalum kutoka nchini wawawezi kuruhusiwa kufanya kazi katika mataifa ya kigeni. Serikali iaanzishe mchakato wa kufufua viwanda ambazo ziliporomoko , wakifanya hivyo vijana wetu watapata ajira na ufisadi itapungua kamwe .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img