3.1 C
London
Wednesday, January 22, 2025
HomeCommunityUgonjwa Wa Macho Mwekundu Mombasa

Ugonjwa Wa Macho Mwekundu Mombasa

Date:

Related stories

Why Emotional Literacy Matters for Children

Building a Strong Foundation: Why Emotional Literacy is Essential...

Mind Management, not Time Management.

The Illusion of More Time: Why Mind Management Trumps...

Behaviour Management in Children

Understanding and Guiding Children's Behaviour: A Practical Approach Raising children...

What’s New in the Latest ChatGPT: Enhanced Features and Capabilities

The latest version of ChatGPT, powered by GPT-4, has...

The Silent Revolution: How Tech Schools Are Transforming Lives in Nairobi’s Slums

In the heart of Nairobi’s bustling informal settlements, a...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Maambukizi ya Ugonjwa wa macho Mwekundu (Red eye) unaonekana kusambaa kwa kasi katika kaunti ya Mombasa. Watu wengi wamejawa na wasiwasi chungu nzima . Wakazi mjini Mombasa wamesisitiziwa kuchukua tahadhari na kudumisha usafi wa mwili na mazingira.Usafi wa kibinafsi inahusisha kuoga, kukata kucha, kupiga deki nyumba zao na pia kuosha vyoo viwe safi. Usafi wa mazingira inahusisha kufyeka nyasi, kunywa maji safi na kuchoma takataka. Ugonjwa wa macho Mwekundu unaweza kusambaa katika Shule. Wakati huo virusi husamba kwa Kasi , virusi hivi huwa maeneao ya darasani ni viumbe wa Red eye husamba kwa haraka sana.

Bila shaka, serikali ya kaunti ya Mombasa inawataka wazazi wawazuia watoto wao nyumbani , wale wenye macho mwekundu ili kudhibiti, kuenea kwa ugonjwa huu hatari. Si ajabu kufahamu kuwa kuna hofu kuwa ugonjwa huu imesamba kutoka taifa jirani la Tanzania, ambako zaidi ya visa mia nane vimeripotiwa na huko Mombasa sasa kukiwa na zaidi ya visa elfu moja ya walioathiriwa na Ugonjwa huu.

“Conjunctivitis” pia unajulikana kama Ugonjwa wa macho mwekundu, ambapo huifanya sehemu inayolinda macho huvimba . Kisha inakuwa vigumu kwa binadamu kuona vyema . Imekuwa vigumu wanafunzi kuenda shuleni, kwasababu Ugonjwa huu unaleta utengano kwa wanafunzi.Darasani wanafunzi huwa na wasiwasi sana.Wataalam wa afya nchini kenya bado wanachunguza mlipuko wa maambukizi ya ugonjwa wa macho mwekundu.Unaowasumbua wakazi wa Jiji la Mombasa na Kilifi. Wakazi wa Mombasa wameshauriwa kuzingatia kanuni za usafi kama vile kunawa mikono na kuepuka kutumia vitu vya kibinafsi Kama vile taulo, kuacha kugusa macho kila wakati.

Dalili ya Ugonjwa huu ni kama vile macho kuwa mwekundu, uvumbe, machozi na kuwasha Macho.Wagonjwa wengine hutoa uchafu kutoka kwa jicho kwa mujibu wa maofisini wa afya katika kaunti ya Mombasa.Ugonjwa wa macho mwekundu husambazwa na bacteria baada ya kugusana na mtu anayeugua tayari. Bi Muthoni amewataka wananchi katika kaunti ya Mombasa kudumisha kiwango cha juu Cha usafi, kujiepusha na wake wanaoambukizwa , si lazima kujitenga na wale walioambukizwa, huku alitoa wito kwa wakazi kutafuta msaada wa wataalamu iwapo wanapata dalili zozote za ugonjwa huu.

Ni Bora kutahadhari kabla ya hatari si rahisi kudumisha maagizo haya, lakini ni bora kuzuia kuliko kuponya kwa wakati. Macho pia huwa majimaji na huwasha , Jambo hili hufanya mtu kujikuna, wakati mwingine wanapougua wanaweza kutokwa na matongo meupe au ya manjano.
Mkurugenzi wa afya daktari Khadija Shikelly, ametoa wito kwa wananchi kuimarisha usafi wa mikono ili kuzuia kueneza kwa ugonjwa huu hatari. Alisisitiza umuhimu wa kunawa mikono na kuepuka kutumia vifaa vilivyotumiwa na watu waliougua yaani waathiriwa kwa jumla. Kama unaweza kuvaa miwani maalum ya kuzuia mwanga mkali wa jua, basi unashauriwa kuitumia ili kupunguza macho yasiume zaidi.

Mara nyingi maradhi ya macho mwekundu hupona kabisa isipokuwa wachache ambao hupata makovu haya mara nyingi husababisha, changamoto ya kutoona vizuri. Ugonjwa wa macho hufanya mtu kuwa kipofu, Sclera na ngozi ya ndani hubadilika na kuwa nyekundu.

Hali hii husababisha upanuzi wa mishipa almaarufu minuscule ya damu. Macho huvimba na kuonekana mwekundu. Kuna sababu nyingi ya kutokea kwa jambo hili ikiwa ni pamoja na uchovu wa macho. Dallili nyingine ni macho kutoa matongo kwa wingi hasa mgonjwa akiwa amevimba kiasi Cha kushindwa kuona vizuri kwenye mkali wa jua. Maradhi haya huhitaji huduma ya dharura lakini ni Vyema kuhakikisha kuwa mtaalamu wa afya amechunguza ili Kufahamu chanzo kabla ya matibabu kuanza.

Macho mwekundu yanaweza kuonekana ghafla au kwa muda wa ziada. Matone ya jicho husaidia mara nyingi, ikiwa uwekundu hauondoki na unaambatana na dalili zingine, watu wanapaswa kuona daktari.Majeraha ya macho , lensi za mawasiliano na matumizi ya mara kwa mara ya matone ya jicho , husababisha kuwasha na uwekundu, kumsaidia mgonjwa huu ni kuandaa matibabu mapema .

Daktari anaweza kuagiza tiba ya antibiotic ili kutibu maambukizi ya macho yanayosababishwa na bacteria. Dawa nyingi za macho ziko katika mfumo wa matone ya maji kwenye chupa. Kwa mwanafunzi Uongozi wa shule unatakiwa kumshauri mtoto kukaa nyumbani mpaka atakapopona ili kuepuka maambukizi zaidi.

Si vyema kununua miwani bila kumwona daktari, huenda ukasababisha shida , Ugonjwa wa macho isichukuliwe kuwa si hatari ,dalili ya mvua ni mawingu, Wakati unaona dalili zozote basi usinunua dawa, tembelea kituo Cha afya haraka, tusiwe na kiburi kupita kiasi , ilhali macho yetu ndio kioo, binadamu hawezi kuona bila macho, aliye na macho bila shaka haambiwi tazama, huwezi tazama bila macho.Natumai serikali itashughulikia ugonjwa wa macho mwekundu kwa haraka.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img