Furaha ya kila mkenya ni kuishi maisha ya utulivu na amani. Serikali Ina jukumu la kuwapatia wananchi usalamu wa kutosha. Waziri wa usalama kithure Kindiki kila mara anazuru Sehemu mbalimbali za nchi ili kudumisha usalama. Hata hivyo wakazi wa Baringo kasazini walikimbia makao. Utovu wa usalama imekita mzazi. Familia kutoka Kijiji Cha Ayatya, Kagir na Kasile zinaishi kwenye makambi.
Uvamizi wa mara kwa mara kutoka kwa wezi wa mifugo, iliwafanya kukimbilia usalama wao. Wakazi wa Baringo hawa chakula na wanakabiliwa na hatari ya kuathiriwa na magonjwa. Shida kubwa katika maeneo ya Baringo ni njaa, hali ya mvua kutonyesha kwa muda. Kuna baridi kupita kiasi lakini wenyeji hawana makazi. Inaelekea miezi mitatu wakazi wakiwa wanaishi kichakani.
Aidha watoto wamelazimika kuacha masomo yao, ambapo wanahofia maisha yao ya baadaye yataathiriwa. Idadi ya watoto ambao hawaendi shuleni ni kubwa mno. Watoto hawa hawawezi kuzungumza . Afisa mkuu wa shirika la “New Dawan of Hope” Bi Joan Jemutai amewaomba wahisani wajitokeze ili kuwapatia wakazi chakula. Ni jambo la kushangaza mno, wakazi wa Baringo wanaugua magonjwa ya malaria ambao husababisha na kuumwa na mbu.
Ni vyema mashirika mbalimbali kama makanisa, hospitali au shule kujitolea kuwasaidia wakazi hawa. Zaidi ya familia mia moja imetoroka makao kwasababu ya wavamizi wa mifugo.Jamii za wafugaji hutegemea wanyama kama kitega uchumi.
Katika kaunti ya Mombasa wakazi wanaishi kwa hofu zaidi.Hii ni baada ya genge hatari kuchipuka, sehemu za Mshomoroni, Likoni na kisauni zimeathiriwa zaidi. Watu arobaini wameripotiwa kuuawa na magenge ya kihalifu. Katika kipindi Cha mwaka mmoja , huku washukiwa thelathini wamekamatwa na maafisa wa polisi. Magenge haya hatari huvamia wakaji wakitumia visu , panga, na hata shoka. Wafanyibiashara wameibiwa huku wakijeruhiwa. Ni nyema kwa serikali kujitolea kurejesha amani katika maeneo ya Kisauni. Wakazi wameamua kuhamia katika sehemu salama. Ni jambo la kushangaza kuona kuwa wafanyibiashara wamepoteza mali yao lakini polisi wamenyamaza kimya.
Gavana wa Kakamega bwana Fernandez’s Barasa anaomba uchaguzi ufanywe kwa haraka sana. Hii ni baada ya magenge ya hatari kuvamia bawabu , Kisha kumuua. Kifo Cha bawabu huyu liliwashangaza wengi . Bawabu ni mlinzi wa kibinafsi ambaye huchunga mali ya watu . Ikiwa tutakuwa na utangamano kati ya polisi na raia basi visa hivi vitapungua . Aidha kule kitale Kuna bawabu aliwauwau na magenge ya wezi , lengo lao ilikuwa kupora mali Kisha kutoroka, bado serikali inafanya uchunguzi kuhusu suala hili.
Katika kaunti ya Busia Kuna kikundi Cha “Jobless Corner” kikundi hiki kinawaangaisha wakaji zaidi. Katika kaunti ya Nakuru maeneo ya Molo magenge ya majambazi yanawaangaisha wakazi kwa kuiba mifugo na mali. Kikundi Cha “Jobless Corner “kimekita mizizi eneo ya Marachi . Vijana wanatembea na panga wakati wa usiku. Gavana wa Busia bwana Paul Otuoma anawarai wakaji kutoa ripoti kuhusu kikundi hiki . Rais William Ruto alipokuwa Busia aliwaonya vijana hawa kuhusu ushambulizi wao.
Waendeshaji pikipiki mjini Busia wamepoteza maisha yao . Wale ambao hutekeleza mauaji ni kikundi hiki Cha “Jobless Corner” ombi langu ni kuwa serikali itawanusuru wakaji wa Busia kwa haraka. Isitoshe seneta wa Busia mheshimiwa Okiya Omutata alivamiwa nyumbani kwake . Magenge haya yalimjeruhi shemeji wa seneta huyu, ilikuwa bahati nzuri , usiku huo , seneta huyo hakuwa nyumbani kwake, kiongozi huyu amepitia masaibu mengi sana .Ofisi yake katika kaunti ya Busia ilivamiwa na magenge ya wezi , Kisha kuharibu mali yake. Pia Kuna wakati seneta huyu alipata ajali maeneo ya Kisumu .Je, ni nini kinasababisha magenge ya wezi kuchipuka ? Mbona wao hujeruhi watu na kuiba mifugo.Magenge haya hukosesha wenyeji amani . Ni wazi kuwa vijana wengi kule Kijijini hawana kazi.Wengi wao hutegemewa na familia zao . Ili kupata riziki kwa njia ya mkato .Wao huamua kujiunga na magenge haya hatari.
Mara nyingi magenge yalianza yakiwa vikundi vya vijirani . Watu waliokuwa katika umri wao wa utineja wa mapema waliokusanyika katika mtaa . Walifanya mambo pamoja kisha wakaungana ili kujilinda na kikundi Cha karibu kikundi chao kikaanza kudidimia na kuwa chenye ujeuri kama washirika wake na kikahusika katika utendaji wa jinai ulio hatari. Genge la upinzani kutoka mtaa Mwingine huenda likiona kikundi hiki kipya kuwa adui kwake. Masaibu ya wakimbizi samburu, wakazi wametokea kuwa majangili na kuishi kwenye kambi ya Longewan. Katika kambi hii maisha ni magumu ni sana, wanaiomba serikali kuhakikisha kuwa Kuna usalama ili waweze kurudi nyumbani kwao.
Majangili hawa walimua mwakilishi wadi Angata Nanyukie , Paul Leshimpiro. Katika kaunti ya Kisumu eneo la Alungo magenge ya wahalifu yalivamia na kuibia wakazi. Majambazi hawa hudai pesa ikiwa utawanyima wanateketeza nyumba yako .
Ukosefu wa udugu wa familia, mazoezi ya kinafsi , ni kielelezo thabiti Cha dalili yanayochangia kuchipuka kwa magenge haya. Televisheni na sinema ambazo watoto hutazama huchangia wao kuwa jeuri. Ni vyema kuwafundisha vijana maadili ili waepuke magenge haya hatari .