3.2 C
London
Friday, November 22, 2024
HomeEducationJE MTAALA MPYA WA CBC INA FAIDA ZIPI?

JE MTAALA MPYA WA CBC INA FAIDA ZIPI?

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Nani asiyependa mabadiliko? Je, ni Bora jamii kuwa na mwekekeo mpya, haya ndiyo maswali wanafunzi , wazazi na walimu hujiuliza kila siku. Mtaala hurejelea seti ya ujuzi na uzoefu wa masomo . Baada ya mtaala wa nane nne nne kukamilika mwaka wa elfu mbili na ishirini na tatu , mtaala wa umilisi bila shaka ukaanza kukita mzizi.

Ifuatayo ni faida ya mtaala wa umilisi katika nchi ya kenya . Katika lugha ya kingereza mtaala huu huitwa “CBC” . Wanafunzi hujifunza kuhusu maliasili . Maliasili ni vitu vinavyopatikana katika mazingira kama vile misitu , wanyamapori , bahari , maziwa na madini. Makavazi ya “fort Jesus” hisaidia wakenya kutangamana na watalii kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni. Maliasili yameiwezesha kaunti ya Mombasa kipiga hatua kimaendeleo kutokana na mapato ya utalii.

Wanafunzi hujifunza kuhusu aina mbalimbali ya magonjwa yasiyoambukizwa kwa mfano pumu, saratani , kusukari , kifafa na kiharusi, ni magonjwa ambayo hayasambazwi kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine . Magonjwa haya yanaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula visivyofaa. Matumizi ya vileo na dawa za kulenya , kutofanya mazoezi ya , viungo vya mwili , majeraha kama ya ajali na hata matatizo ya akili.

Kujifunza kuhusu majukumu ya kijinsia . Katika jamii Kuna majukumu mbalimbali kwa mfano kulea , kupika , kujenga nyumba, kuosha vyombo, kulima , kupiga deki na hata kufagia nyumba. Kupitia somo la sayansi ya nyumbani jinsia zote hujifunza mbinu mbalimbali za kuanda vyakula vya aina mbalimbali. Kupitia somo la kilimo jinsia zote hujifunza mbinu mbalimbali za kukuza mimea shambani.

Majukumu haya yote huwasaidia wanafunzi kuwa na maarifa maishani mwao. Huduma kwa jamii. Mtaala wa umilisi umewasaidia wanafunzi walemavu kupata ujuzi kama vile useremala , ushonaji na uhandisi , kuwasaidia walio na mahitaji maalumu. Kumbuka kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu Wana vipawa vya kipekee. Kuishi na ulemavu si kutojiweza Bali ni kubarikiwa kwa njia tofauti na wengine . Kuna baadhi ya Mambo watu wenye ulemavu wanaweza kufanya.

Heshima kwa tamaduni zetu. Heshima si utumwa . Ni bora kuheshimu wazazi wetu kila mara. Darasani wanafunzi wanapotangamana wa wengine, wakiheshimiana kila mara vita na chuki itapungua . Watafanya zoezi kwa furaha. Ikiwa Kuna tofauti mahali , Haina haja kukashifiani , tuziheshimu tamaduni zetu na kuzitunza kama tulivyokuzwa katika jamii yetu na walimu wetu darasani.

Mahitaji ya kiteknolojia na ya viwanda . Elimu nchini kenya inafaa kuwapa vijana stadi na mielekeo inayohitajika , kwa maendeleo ya kiviwanda . Kenya inatambua madiliko ya haraka ya kiviwanda na kiteknolojia yanayofafanyika hasa katika ulimwengu ulioendelea . Tunaweza kuwa sehemu ya maendeleo haya ikiwa mfumo wa elimu unalenga kumsaidia mwanafunzi apate stadi na mielekeo itakayotayarisha vijana kwa mabadiliko yanayoendelea ulimwenguni.
Mtaala wa umilisi hutoa nafasi ya kujiendeleza na kujitosheleza. Elimu inapaswa kuwezesha kutambua, kukuza na kuimarisha vipawa vya kila mmoja ili kuweza kujiendeleza na kujitosheleza. Inafaa kuwawezesha watoto kukuza uwezo wao. Kipengele muhimu Cha maendeleo ya kibinafsi ni ujenzi wa tabia ifaayo.

Mahitaji ya uchumi . Wanafunzi Wana malengo baada ya kukamilisha kosi zao. Shuleni . Elimu wanayopata inapaswa kukuza raia walio na stadi maarifa , ujuzi za kibinafsi zinazohitajika katika maendeleo ya kiuchumi. Katika gredi ya sita na saba . Mwanafunzi anasoma somo la biashara . Somo hili hujenga uchumi huru na wa kisasa ambao unahitaji wafanyikazi wa kutosha. walio na maarifa yanayohitaji humu nchini.

Kustawisha mwekekeo chanya kuhusu afya Bora na uhifadhi wa mazingira. Elimu inakusudiwa kujenga mielekeo ifaayo miongoni mwa vijana kuhusu udumishaji wa afya Bora . Na mazingira kwa kujiepusha na mienendo inayoweza kudhuru afya ya mwili na akili.
Aidha inafaa kuimarisha mielekeo chanya kuhusu ukuzaji wa uhifadhi wa mazingira wa kuwaelekeza vijana kuthamini usafi mazingira. Ndiyo maana Rais William Ruto anahimiza wakenya kupanda miti. Hata katika gredi ya tatu wanafunzi waliende kufagia sokoni ili kudumisha usafi . Jambo hili litawasaidia kuwa wabunifu kule Kijijini.

Kupitia somo la kiswahili na kingereza ni wazi kuwa mwanafunzi atajenga uweza wake wa kuwasiliana na kuhusiana katika jamii. Elimu itamwandaa kwa ulimwengu na kazi. Mwanafunzi atapata maarifa ya kijamii na kitamaduni . Ataweza kujiekeza na vilevile kupata fursa ya kutoa huduma kwa jamii.
Hata hivyo ikiwa serikali ya kenya itatilia manani upungufu wa C.B.C. yaani mtaala umilisi kama vile uhaba wa walimu , kupunguzia wazazi gharama ya kununua vitabu , kuboresha miuondo misingi na kupunguza idadi ya masomo darasani. Bila shaka mtaala huu utawasaidia wanafunzi wengi kuwa na ujuzi kikamilifu na kijiajiri baada ya masomo.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img