5.5 C
London
Wednesday, November 27, 2024
HomeCommunityUSAWA WA JINSIA

USAWA WA JINSIA

Date:

Related stories

Nurturing Talent; Kenya’s Path to Unlocking Its Greatest Asset

In a country brimming with vibrant creativity, boundless energy,...

The National Examination Theft; A Breach of Trust and Integrity.

In a startling turn of events, Kenya's education sector...

The University Lecture Strike; A Dilemma for Students

As the new academic year begins, universities across the...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes


Mtoto wa kike ua kiume ana haki zake katika jamii husika . Hata hivyo mtoto wa kiume amedunishwa zaidi katika jamii. Nafasi ya mtoto wa kike katika jamii ni kubwa zaidi .kwa Nini watoto wa kiume amekosa mashauri na maelekezi .

Katika serikali nyingi ya miradi na hela nyingi zimetengewa mtoto wa kike. Nafasi ya mwanamke imetiliwa mkazo , katika kaunti ya Nakuru wanawake wengi walipata nafasi ya Uongozi , kule homabay Gavana Gladys Wanga , Nakuru Susan kihika na mwakilishi wa wanawake kule Bomet mweshimiwa Linet Toto ni jinsia ya kike . Kwa kweli wanawake ni wengi Uongozini.
Mashirika mengi yamebuniwa kutetea mtoto wa kike na wanawake. Kwa mfano chama Cha maendeleo ya wanawake ilikashifu mauaji ya scarlet wahu, aliuawa , wananake wengi walijitokeza kukashifu kitendo Cha ugaidi Cha mauaji. Kule Nairobi kulikuwa na maandamano .

Alama za wasichana kuingi vyuo vikuu zimeshushwa kiasi . Ingawa Kuna haki za watoto , na pia mtihani hufanywa kwa usawa. Serikali kwa mara nyingi hupendelewa jinsia ya kike na kumwacha mwanaume akijitafutia kupitia kwa kazi za sulubu kama mjengo. Ni wazi kuwa jinsia ya kiume imebaguliwa.
Shule za mabweni za wasichana ni nyingi mno ilhali mtoto wa kiume ameachwa kumezwa na magenge kama vile munguki na pombe haramu. Si ajabu kusikia naibu wa Rais bwana Rigathi Gachagua, akipiga vita uuzaji wa pombe Kijijini. Katika kaunti ya kirinyaga, pombe hii haramu iliua watu zaidi ya ishirini na tatu . Poleni kwa familia hizi kuwapoteza wapendwa wao.
Mtoto wa kike amependwa zaidi . Wakati jamii nyingi inamtetea mtoto wa kike ilhali mtoto wa kiume ameachwa kumezwa na ulimwengu ajiamulie hatima bila mtetezi wa moja kwa moja . Jambo hili huwafanya watoto wakiume kuwa na hasira kupita kiasi.

Hata hivyo mtoto wa kike amedhalilishwa kwa njia zifuatazo. Hapo zamani za kale mtoto wa kike akipata Mimba alikuwa anafukuzwa shuleni. Hali hii inamfanya mtoto wa kike kukosa kuhudhuria masomo kikamilifu.
Jambo la ukeketaji imegonga vyombo vya habari nchini kenya . Katika kaunti ya samburu, bado wasichana wanakeketwa . Mtoto wa kike anapashwa tohara kwa lazima bila hiari.

Tamaduni ni Mila imekita mzizi mno . Katika jamii ya waluo bado mume akifariki , mke alirithiwa na shemejiwe mume anapoaga Dunia
Ubabe dume ulikita mzizi katika jamii. Ubabe dume ni Hali ya kupenda wanaume zaidi ihlali kumchukia mwanamke, wakati mume amefariki, mwanamke hakuruhusiwa kupata urithi wa wazaziwe na mumewe.
Mtoto wa kike anafanyishwa kazi nyingi za nyumbani husasan za jikoni. Ni Bora kufahamu mtoto wa kiume ananunuliwa vifaa vya kucheza kama gari au ndege, kumtayarisha kuwa rubani. Ilhali mtoto wa kike hununuliwa mwanaserere huku akitayarishwa kuwa Yaya , huku akibebe mtoto huyu . Watoto wa kike wanapoolewa mara nyingi hupigwa na wanaume wao. Jambo hili hutokea wakati Kuna migogoro ya kifamilia. Vita hivi kwa mara nyingine huweza kusababisha vifo au hata ulemavu wa viungo vya mwili kupitia mapigo haya kila siku.

Mwanamke ananajisiwa na kuharibiwa jina katika jamii .si kila mmoja hufurahia maendeleo wanayofanyia jamii. Hata wakati wa siasa , wao hutukamwa wakati wanafanya kampaini zao. Kwa mfano Gavana na Meru alipokumbwa na Kasi ya kutaka kuondolewa madarakani . Alikashifiwa na wanaume kupita kiasi . Tusisahau mwanahabari Monica kimani aliwauwau kwa njia tatanishi , bila kutarajia . Serikali inafaa kuweka mikakati zaidi kuzuia vifo hivi kuwapatia vijana .

Katika jamii husika, mtoto anapozaliwa kila mmoja Huwa na furaha kupita kiasi . Matarajio ya wazazi ni kuwa watoto huleta mwelekeo mpya , na pia wao hubadilisha sura ya jamii. Katika kaunti ya samburu, Turkana na hata Narok. Watoto wa kike wanaozwa mapema Tena kwa wazee , ambao wamewazidi umri. Wazazi huwaoza watoto wao wa kike kwasababu ya umaskini. Mtoto wa kike atasalia kuwa nyuma kielimu , mwishowe kuishi maisha ya uchochole.
Mwanamke amesahaulika kwa miaka mingi mjini. Katika jamii ya maasai wanawake ndiyo huchunga ngo’ mbe na mbuzi. Hii ni njia moja ya kudharau wanawake.

Kuna baadhi ya kazi ambazo wanawake hawawezi kufanya kwa urahisi. Kwa mfano kuchimba kisima na kujenga nyumba. Ingawa kila jinsia Ina haki zake ,ni Bora kuwaheshimu pamoja na tamaduni zao .
Mtoto wa kiume umesahaulika katika jamii kwa kiasi kikubwa. Mambo mengi anajifanyia bila kupata ushauri na maelekezi. Lazima serikali ivulie njuga suala la jinsia zote bila ubaguzi. Ulifanya hivyo , jamii nzima itakuwa usawa. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu .

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img