4.1 C
London
Thursday, January 2, 2025
HomeCommunityUVUTAJI WA SIGARA NA MADHARA YAKE

UVUTAJI WA SIGARA NA MADHARA YAKE

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Je, ni muhimu binadamu kivuta sigara maishani mwao? Mbona binadamu kila mara avute sigara ? Watu wengi bado wanajiuliza maswali mengi akilini mwao. Ni Bora kufahamu sigara ni nini na kwasababu zipi binadamu anapenda kivuta sigara . Sigara ni kuvuta Cha uraibu kinachotengenezwa kwa tumbaku na kusokotwa karatasi ya aina maalum , chenye umbo refu na la mviringo. Sigara huleta madhara yafuatayo kwenye mwili wa binadamu anapovuta kila wakati.

Ugonjwa wa moyo . Wataalamu wa sayansi na madaktari wamefanya bidii na kuthibitisha ukweli kuwa Moshi wa sigara huathiri wavutaji wa sigara na watu walio karibu nao na pengine huleta Ugonjwa wa moyo . Si ajabu kuwa wavutaji hupatwa na kikohozi Cha daima kisichosikia dawa kamwe.

Jambo hili husababisha Ugonjwa Wa “pumu ” kutokana na Moshi wa sigara unapoingia ndani ya mapafu ya mwanadamu ni hatari mno. Kemikali zilizo ndani ya sigara si nzuri Kwa afya ya binadama. Huweza bila shaka kusababisha saratani . Dalili za Ugonjwa wa saratani ni kukohoa damu na maumivu kifuani. “Saratani” ya mapafu , ni Ugonjwa sugu ambao umewaua baadhi ya wakenya wengi . Moshi ya sigara kwa mara nyingi hutoboa mapafu. Uvutaji wa sigara husababisha vidonda vya tumboni ambayo Huwa vigumu kutibu.

Na kupona , kwa hivyo wakenya wenzangu ni bora kuchukua tahadhari kabla ya hatari ili kujiepusha na magonjwa yanayotokana na uvutaji wa sigara.
Kemikali zinazopatikana ndani ya sigara hupunguza uwezo wa ngozi kunawiri hivyo huanza kuzoeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika . Si ajabu kuona mvutaji wa sigara kuonekana mkongwe zaidi ya umri wake . Kule Kijijini utawapata wazazi wanajiuliza maswali mengi .

” Kwa Nini mtoto wangu anazoeka haraka sana ?’Mbona ngozi yake Haina afya Bora kama mtu wa kawaida ? Jawabu ni kuwa madhara ya sigara si Bora kwa afya ya binadamu.

Kila mzazi anafuraha wakati watoto wao hufurahia lishebora. Kule shuleni walimu hutoa elimu kuhusu madhara ya sigara, lakini haya yote Huwa wanapuuza. Uvutaji wa sigara huchangia kwa asilimia kubwa kudhofika kwa Kinga za mwili . Watu wanaovuta sigara hukosa hamu ya chakula . Hata kama chakula ni kitamu kupita kiasi. Tatizo hili kwa mara nyingi huwadhofisha kiafya. Chakula Huwa ni vigumu kwao kuwa Cha muhimu.

Sigara humfanya mtu kupoteza unadhifu wa mwili. Kinywani kila mara hutoa harufu mbaya na kuozea kwa meno . ” Nani hupenda harufu mbaya?” Utawapoteza marafiki wengi kwasababu ya harufu mbaya mdomoni. Pia mabinti hukerwa na wanaume wenye kunuka Fe kwenye kinywa wakati wanapoongea.
Uchafu wa sigara si nzuri kwasababu huganda kwenye kucha na baina ya vidole vya mvutaji sigara . Uchafu huo hubadilisha rangi ya vidole na kucha za binadamu .

Ngozi ya vidole hukaukana kuwa ngumu kwasababu ya joto na kemikali za sigara.
Wakati wa kufanya mazoezi ya kukimbia mfupa wa binadamu Huwa na nguvu zaidi. Lakini wakati wa unavuta sigara kwa muda mrefu mifupa Huwa miepesi ,na kupunguza nguvu itokanayo na msukumo. Sababu ni kuwa kemikali zilizoko ndani ya sigara hupunguza madini yanayotengeneza mifupa iliyo na nguvu za kustahimili uzito wa mwili. Baadhi ya watu huvuta sigara na kutupa Vipande vya sigara ovyo bila kuzimwa na hivyo husababisha hasara kubwa kama vile uchomaji wa misitu , nyumba. Au nguo na wakati mwingine hata si ajabu kusababisha vifo. Uvutaji wa sigara imefikia kiwango Cha kutilia shaka zaidi. Tusipozipa ufaa bila shaka kutajenga ukuta.

Utaona vijana yaani wasichana kwa wavulana wadogo sana wakivuta sigara mbele ya watu wazima bila kujali.
Hii ni aibu kubwa sana kwa wazazi . Tabia hii inatokana na mifumo mbaya wanayoiona kutoka kwa wazazi wao pamoja na mitandao. Si ajabu kusikia akimtuma mwanawe amnunulia pakiti ya sigara dukani. Jambo hili likiendelea wazazi kama Hawa huwafanya watoto wao kuwa na mazoea ya wao kivuta sigara ili wao wajione kuwa wao pia ni watu wazima.

Vijana wengine huvuta sigara ili wapate fahari au heshima . Wanadhani ni njia Bora ya kujenga mwili wao , ajabu ni kuwa wanaharibu mwili wao . Katika television au runinga ni vyema kujua kwamba sigara hazifai kupatiwa matangazo ya kuvutia vijana kwenye runinga.

Aina nyingine ya uraibu ni Bangi .je, unafahamu Bangi ni nini? Mbona vijana wa Karne ya sasa wanavuta Bangi . Kwani hawana Elimu ya kutosha shuleni? Bangi ni aina ya mimea inayolenya na kupumbaza akili ya mwanadamu. Bangi kwa mara nyingi huwa inatafunwa . Vijana wanatumia Bangi wao hukonda kama ngonda na wasijua wanachokifanya.wanasayansi wamethibitisha kuwa Bangi huharibu kituo Cha kifikira na kumfanya mtu kuwa kama mwendawazimu .
Ni vyema wazazi wawakanye watoto wao kuwa ni vibaya na hatari mno kutumia Bangi na sigara.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img