10.4 C
London
Saturday, December 21, 2024
HomeInternationalKENYAWATU WENYE MAHITAJI MAALUMU

WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU

Date:

Related stories

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities

We Must Bring Digital Literacy to Remote Communities In the...

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Katika jamii Kuna watu wa aina mbalimbali. Kuna watu ambao ni wazima , wengine Wana mahitaji maalumu. Wanaishi na upofu , ububu , uziwi na hata ulemavu wa viungo vya mwili.

Kipofu ni mtu asiyeona kutokana na kuugua ajali au kuzaliwa hivyo. Ububu ni Hali ya kutoweza kusema kwasababu ya kiziwi au kuwa na kasoro ya ulimi ,kinywani au tabia ya kutopenda kuongea.kuna wale waliopata matatizo haya kutokana na ajali barabarani kama vile kugongwa na gari au pikipiki. Wengi hata hupata kasoro hizi kupitia mashambulizi ya vita kama vile alshbab, katika harakati ya kuokoa Mali zao wao hupigwa risasi na hatimaye kuachwa na majeraha mwilini.

Unaweza kuwa mzima lakini upate ulemavu baada ya kupata ajali. Wakati mwingine watu wanapopata matatizo hudhani kuwa pengine dunia imewakasirikia .ulemavu kama polio ni hatari kwa binadamu kwasababu husababisha kupooza kwa viungo vya mwili na mfumo wa hewa.Tusiwadharau watu walio na mahitaji maamumu nchini. Mwenyezi mungu ndiye kutoa vipaji mbalimbali na amewatunuku watu walemavu vipaji vya kipekee. Baadhi Yao huimba vizuri kama ninga wakawa wasanii . Walibobea bila kusahau taaluma zingine mbalimbali ambapo wanetia fora zaidi.

Nchini kenya Kuna waimbaji maalum kama vile Mary Atieno , Solomon Mkubwa , Rose Muhando. Ambao huimba nyimbo za injili , bila kusahau Christina Shusho na wimbo maarufu nashusha nyavu, wasanii Hawa huwabariki watu kupitia nyimbo na maubiri Yao kwa vyombo vya habari
Kunao ambao hawana mkono, lakini ni wachoraji wa kuvutia kwa kushikilia kalamu kwa mdomo au miguu Yao. Walemavu ambao hutia bidii katika kazi zao hufanikiwa maishani. Wao huishi maisha ya Raha kama ya mfalme anayemiliki himaya kubwa ya kifahari.

Jukumu la kila mzalendo ni kutoa mchango wake kuwafaa watu wakati wanapotekekezwa , wao huishi Maisha ya upweke. Ni vyema kila mkenya kuwaonyesha walemavu upendo . Kama wanadumu wengine ili wajihisi kuwa katika sehemu ya jamii. Utu huu utawafanya kufurahia na kupunguza huzuni na vilio. Tusisahau mheshimiwa Tim Wanyonyi ni mlemavu japo anachapa kazi kwa bidii.

Watu wenye mahitaji Maluma wanahitaji msaada kutoka kwa jamii na serikali. Watu katika jamii wanaweza kushirikiana kujenga vituo vya kuwasaidia watu Hawa. Kila jamii Ina mafundi na maseremala . Hivyo shughuli hii inaweza kufanywa kwa urahisi. Bila malipo . Serikali inaweza kuchangia kwa kuwatuma wataalamu kufunza taaluma mbalimbali katika vituo na taasisi hizo. Watu Hawa watafaidika na kujikimu maishani.

Kwa mara nyingi , walemavu hupitia shida nyingi wao Huwa wametekelezwa na wazazi wao na wakaokolewa na wasamaria wema. Njia Bora ni ya kuwahudumia watu Hawa ni kuwapatia mavazi, vyakula na vifaa vya kuchezea . Kanisa pia hujitolea kuwanunulia vitimaguru. Wengine hutoa pesa ili kuwanunulia walemavu , mahitaji ya kimsingi kama vile sabuni , mafuta ya kujipaka , mswaki na dawa ya meno.
Walemavu wanafaa kutiwa moyo na kushauriwa kuhusu umuhimu wa kuweka mazingira safi. Mazingira ni vitu ambayo hutuzunguka . Jukumu la kila mkenya ni kudumisha usafi. Unapowatembelea walemavu ni vyema kuchukua vifaa kama kwanja almaarufu ” slasher” kufyeka nyasi au hata kusafisha mazingira Yao kila mara.

Ikiwa una zawadi wakabidhi kwasababu kutoa ni moyo usambe ni utajiri .walemavu wanahitaji huhitaji kutiwa moyo kwa kupiga picha nai .Isitoshe kukula pamoja nao. Ni vyema kufahamu kuwa si lazima yawe ulemavu tu. Kuna mengine kama vile zeruzeru ambao huweza kuwa na matatizo ya macho. Huwa wanastahimili mwangaza mwingi.

Hivyo basi zeruzeru wengi wao huvaa miwani ya kupunguza nguvu za mwangaza . Katika Hali ya kuwafaa darasani vizuri mwalimu awaweke wanafunzi Hawa karibu na ubao , mbali na mwangazi mwingi. Kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawasikii vizuri au hawaoni vizuri . Ni Bora wanafunzi Hawa pia kuketi sehemu ya mbele ya darasa ili kuweza kushiriki kikamilifu katika masomo.

Cha msingi zaidi ni kuwakabili jinsi walivyo na kuwasaidia kikamilifu katika masomo wakati wanahitaji msaada maalum . Wanapotangamana na wenzao na kufanya kazi pamoja . Wao huanza na kuteleleza shughuli zao ipasavyo katika jamii husika.

Nchini kenya shule za walemavu ni Bora ziwe. Na vidato vya kupandia . Upande mwingine kuwa na vijia vya kuwasaidia wanafunzi ambao wanahitaji kutumia vitimaguru kuingia darasani. Vyoo vijengwe kwa kuzingatia wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Serikali imepiga hatua katika kuandaa shule na taasi ambazo zimepewa mafunzo watu wenye mahitaji maalumu. Tusisahau kuwa watu wenye changamoto maalum Wana vipaji vya kipekee maishani.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img