12.1 C
London
Wednesday, October 30, 2024
HomeCommunityUmuhimu Wa Madini

Umuhimu Wa Madini

Date:

Related stories

Youth Employment turn in Online Work

In a digital revolution, many young people are finding...

Early Marriages and Teenage Pregnancies in Kenya

Early marriages and teenage pregnancies are significant problems in...

RISING UNEMPLOYMENT OPPORTINITIES IN KENYA

Unemployment is a growing issue in Kenya, affecting many...

CRIME RATES INCREASE IN NAIROBI

Nairobi, June 18, 2024 - Crime rates in Nairobi...

Concerns Rise Over Increasing Number of Street Families in Nairobi

In Nairobi, Kenya’s capital city, concerns are growing over...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Madini ni uti wa mgongo wa nchi. Kuna aina mbalimabali ya madini kama vile zinc, dhahabu, shaba na kadhalika. Madini Ina faida kama vile kuimarisha mbegu za uzazi. Kiwango cha zinc cha kutosha humwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri. Biashara ya uchimbaji migodi hufanyika Katika kaunti kadha kama kwale,Migori, Kisumu na hata Busia.

Hata hivyo wachimba madini hupitia shida nyingi sana ikiwemo kifo. Katika Kaunti ya Migori wachimbaji watano wa madini waliaga dunia, baada udongo kuporomoko. Mvua ilinyesha kupita kiasi katika kaunti ya Migori. Taarifa hii ilidhitibishwa na Gavana wa Migori mheshimiwa Ochilo Ayacko. Serikali imeamuru kusimamamishwa kwa shughuli zote za wachimba migodi kule Migori. Waziri wa usalama mheshimiwa kithure Kindiki alisema haya baada ya kufanya mkutano na kamati ya usalama.

Vilevile wachimba kutoka Migori wamemrai Waziri wa usalama wa ndani, kubadilisha agizo la kufungwa kwa shughuli za kuchimba migodi.Muungano wa wachimba migodi wakiongozwa na bwana Dan Odida anasema kuwa , agizo hili lilitolewa bila kufanya mazungumzo . Wafanyikazi katika uchimbaji wa madini wanapitia shida nyingi.Wao hutegemea madini ili kulisha familia zao, kwa hivyo wamekosa mapato yakutosha kuwapeleka watoto wao shuleni.

Isitoshe katika kaunti ya Busia wafanyibiashara wanaoendesha shughuli za uchimbaji dhahabu katika Kijiji Cha Bumutiru , hawana furaha tena, hii ni kwasababu ni lazima watume maombi ya leseni upya. Agizo hili limetolewa na waziri wa usalama wa ndani . Katika eneo la magharibi ya kenya wengi ambao wanajihusisha na kazi hii hawatumi vifaa bora vya kujikinga dhidi ya kazi hii nzito hatimaye imewafanya kuangamia iwapo maporomoko ya ardhi yanatokea.

Shughuli za uchimbaji madini haramu zinaweza kusababisha uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na ukataji miti , mmmonyoko wa udongo na uchafuzi wa maji, Athari hizi mbaya za mazingira zinaweza kuzuia watalii wanaotafuta maeneo safi na endelevu. Madini ni taaluma ya kisayanasi ambayo inahusika na vipengele ikiwemo ni pamoja na mali na kioo Cha jamii.Uchambaji madini mara nyingi huchukuliwa kuwa sekta maalum inayohusisha jumuiya zilizounganishwa kwa karibu na wafanyikazi wanaofanya kazi .

Nchini kenya madini ya coltan hutumika kutengeneza betri ya magari ya umeme , simu za mkononi na vifaa vya kielekroniki.Madini haya yapo kila mahali katika mazingira yetu , kila jiwe limeundwa na madini. Ardhi ya shamba Ina kiwango kikubwa Cha madini , madini kadhaa hupendwa zaidi Kama vile johari, mawe ya thamani.
Rais William Ruto alitoa onyo Kali kwa wachimba madini nchini, wanaoendesha shughuli zao kinyume na Sheria, sera ya madini na rasilimali ni vyema kutambulika ikiweko mifumo, kanuni na mikakati ya kutoa utafutaji na uvunaji wa madini , tofauti kama vile kawi ya mkaa , lakini bado inaorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayoendelea kuwa kiuchumi.

Wasimamizi wa mgodi kwa ushirikiano na serikali wamepata Mafunzo. Wachimba migodi wanapaswa kuzingatia usalama wao, kwanza kabla ya kujitosa katika biashara ya madini .Ni bora wawe na leseni rasmi kutoka kwa serikali kuu au serikali ya kaunti. Wachimba madini hufanya shughuli zao kwenye ardhi ya umma ambayo ilifaa kujengwa Shule jambo hili ni hatari.

Athari ya mazingira ya uchimbaji madini inaweza kuwa kubwa na ya kudumu kwa muda mrefu .Kuna mifano utendaji mzuri na mbaya . Kushuka kwa madaraja ya madini, gharama kubwa za matibabu, ubinafsishaji na urekebishaji, Upya imechangia kupunguza gharama ya madini na kuongeza tija zao.Katika uchimbaji wa madini ni kama bahati yako, jinsi ilivyo mchezo wa kamari unaweza toka miezi mitatu bila kupata chochote.

Wakazi wa Karibuni, kaunti ya Kilifi wanafanya kazi ya kuchimba madini aina ya iron katika misitu takatifu ya kaya, hii ni pigo kwa wafanyibiashara wa madini eneo hilo . Nchini kenya, mchakato wa kupata madini ya dhahabu huwa ni ngumu zaidi. Athi river almaarufu (A.R.M) ni kampuni ya kibiashara nchini kenya inayochimba madini na kutengeneza bidhaa kama saruji na mbolea za kilimo .

Madini ya zebaki yaani “mercury” na lead ilipatikana katika sukari , katika kaunti ya Mombasa. Kulitokea malalamishi kutoka kwa umma kuhusu sukari ghushi. Uchaguzi ulibainisha kuwa sukari inayouzwa madukani si salama kwa afya ya binadamu.

Ili kupunguza visa vya wachimba madini wanawake wanapitia mambo mengi katika uchimbaji wa migodi. Ni bora wapatiwe mafunzo kuhusu umuhimu wa afya yao.Bali na madini kuwa na thamani, pia kuna changamoto, wazara ya madini na uchumi wa samawati au bluu , sasa iko katika harakati za kupiga jeki thamani ya Coltan, Madini haya hupatikana katika maeneo mbalimabali kama vile Embu, samburu, Turkana pokot na Tana Tuzingatia Sheria za uchimbaji madini, ikiwa tunataka kuwa salama, katika biashara hii.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img