5.2 C
London
Tuesday, December 3, 2024
HomeCommunityVyakula Vya Kiasili

Vyakula Vya Kiasili

Date:

Related stories

Challenges Facing the Kenya’s Current Socio-Political Landscape

Kenya's current socio-political landscape is shaped by a series...

A Global issue about Female Genital Mutilation

Female Genital Mutilation (FGM), also known as female circumcision,...

Faida Ya Kupanga Uzazi

Upangaji uzazi ni muhimu sana katika familia, inahusu wanandoa...

Madhara Ya Vita Katika Jamii

Hali ya majonzi ilitanda katika kaunti ya Tana River....

Shiquo wa HiStyle: Revolutionizing the Business World with Unbelievable Prizes

In today's rapidly changing business environment, few have managed...
spot_imgspot_img
Reading Time: 4 minutes

Ni muhimu kufanya vipimo vya damu ili kusaidia kupunguza hatari za maambukizi,kwa mujibu wa daktari. Watu hula chakula chocholate bila kuzingatia madhara yake. Ni Bora kuzingatia chakula Cha kiasili. Unapofika umri wa miaka arobaini, ni vyema kupunguza nyama, karanga na siagi, chumvi nyingi si bora kwa afya yako. Matumizi ya limao ni hatari kwa afya yako. Ukiwa na umri wa miaka arobaini ni sharti uwe mwangalifu kwa afya yako kwasababu kadri mtu anavyozeeka anaweza kupunguza uzito. Hivyo ni rahisi kupatwa na magonjwa.

Vyakula vya mtu mwenye umri wa miaka arobaini ni pamoja na samaki, mboga za majani na mzizi kama mringa, matunda, kula uyoga badala ya mayai kila wakati. Ni muhimu kudhibiti matumizi ya dawa za mitishamba au dawa za hospitali bila maelezo ya daktari. Pia ni hatari kiafya kwa mujibu wa daktari. Kula vyakula vya kiasili kama vile mahindi, mtama, mboga na vinginevyo.

Wataalamu mara nyingi huwa wanazingatia faida za lishebora na kiwango cha chakula ambacho mtu anapaswa kula kwa ajili ya afya yake. Hata hivyo lishe bora ina umuhimu kwa mwili wa mwanadamu, tahadhari dhidi ya chakula ambacho watu wanapaswa kula kwa ajili ya afya yako. Vyakula vya kitamaduni vimehusishwa na kupunguza hatari za ugonjwa sugu, kwa vile ugonjwa wa moyo, kisukari na unene uliopitiliza. Vyakula vya kiasili ni kama vitamini nyingi, madini, antioxidants na nyuzi za lishe, ambayo huchangia afya na ustawi kwa ujumla.

Lishebora hutokana na vyakula bora vinavyozalishwa na kuhifadhiwa katika mazingira salama. Watu wanafaa kukumbatia utumiaji wa vyakula vya kiasili, vyakula hivi huongeza kingi mwilini ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kutokea kila mara katika mazingira yao. Njia ya kuboresha afya hata kuongeza wastani wa umri wa kuishi pamoja na lishebora.
Utayarishaji na ugawiji wa chakula unaweza kuleta watu pamoja na kujenga hisia ya utangamano. Sahani za jadi hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, na mapishi ya familia yanathaminiwa na kuwekwa kuwa siri. Ni ajabu sana kufahamu jamii ya kisasa utampata mtoto wa umri wa miaka sita, ana ugonjwa wa moyo. Jamii inafaa kuwahimiza wananchi kukumbatia zaidi vyakula vya kiasili. Waswahili hawakukosea kusema kuwa afya ni taji, hakuna ajuaye isipokuwa mwenye maradhi. Kunywa maji unapoamka asubuhi ni bora kwa afya yako. Si kila wakati kumeza dawa bali kula vyakula vya kiasili.

Watu wanaoishi mjini wengi wao hawatumi vyakula vya kiasili badala yake wanakula vyakula vinavyotengenezwa viwandani na hivyo kuhatarisha afya yao na kufanya mwili wao kudhoofika na hata kukosa nguvu mwilini. Vyakula vya kisasa huwa na madhara kwa afya kutokana na kemikali. Vyakula vya kiasili ni kinga kwa mtumiaji dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ambayo ni tishio kote duniani.

Vyakula vya kiasili husaidia utendaji kazi wa viungo mwilini kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi. Akina mama wa zama hizi, wengi wao wamesahau kupanda mboga za kienyeji, mara nyingi utawaona wakienda sokoni ama dukani kununua mboga. Mboga hizi zinazalishwa kupita mfumo mpya kama sukumawiki, hali inayowasababishia wengi wao kila mara kukumbana na magonjwa kutoka na madhara ya kemikali.

Katika jamii ya kikuyu Kuna mutura wengine huita “soseji ya kiafrika ” ni soseji ya jamii za kenya inayotengenezwa kwa damu pamoja na viungo vingine. Wakenya wengi hupenda chakula hiki, mjini Nairobi utawapata wakipiga foleni, huku wakinunua mutura, mutura huliwa kwa sima na vijana kwa wazee, kule pwani kuna pilau. Chakula hiki ni cha kiasili. Kule pwani mwa Kenya, pilau ni mchele uliopikwa pamoja na vipande vya nyama, kuku, mbaazi, karanga na zabibu. Katika tamasha mbalimbali, Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nasir wameshabikia vyakula hivi kila wakati.

Vyakula vya kitamaduni huambatana na kabila husika. Kule magharibi mwa nchi, ugali ni chakula ambacho hupendwa na wengi nchini kenya. Huliwa sana pamoja na sukumawiki kwa nyama. Mokimo ni chakula kinachoshabikiwa na baadhi ya jamii za kenya. Hutayarishwa kwa viazi rojorojo, mahindi na vitunguu.

Chakula ni nyenzo yeyote yenye virutubisho vinavyotumiwa na binadamu. Vyanzo vikuu vya vyakula ni pamoja na wanyama na mimea. Vyakula vikuu, hutoa kiasi kizuri Cha wanga nyuzi lishe na protini. Vyakula vya kiasili vina virutubisho muhimu kuanzia kwenye ukuaji hadi ujengaji wa ubongo.
Mama lishe na baba lishe hujitokeza kwenye tamasha wakipika vyakula vya asili ya makabila tofauti hakihusishi viungo na mafuta. Chapati hupendwa sana na wakenya wengi. Hutengenezwa kwa kutumia unga wa ngano, chumvi na mafuta. Wakenya wengi huambatanisha chapati na mchuzi au kachumbari ni chakula kitamu zaidi.

Tunaposema tunaimarisha afya bora ya binadamu, lishe inahusika na hapa ndipo tunakuja kwenye vyakula vya kiasili. Mwacha mila ni mtumwa si vyema kuiga chakula cha kisasa na kusahau chakula Cha kiasili.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img