Nchi ni sehemu ya ardhi ambayo imegawanywa kwa mipaka ya kisiasa na inayotambulika kwa jina lake. Nchi yangu inaitwa kenya. Najivunia kuwa mkenya halisi. Dunia Ina nchi nyingi kwa mfano Kenya, Uhabesdhi, Chile, Ujerumani na kadhalika. Mji mkuu wa Kenya ni Nairobi.
Ni Bora kufahamu kuwa Nchi ya kenya hupatikana katika Bara la Afrika upande wa mashariki. Kenya Ina kaunti arobaini na saba kila kaunti ina Seneta. Mwakilishi wa wodi na mwakilishi wa kina mama bungeni. Viongozi Hawa wote huchaguliwa na wananchi debeni baada ya wao kufanya kampaini , kote nchini baada ya miaka Tano.
Nchi yetu imezungukwa na nchi nyingine Tano ambao Huwa majini wa karibu mno. Uhabeshi upande wa kaskazini, Somalia katika upande kaskazini mashariki.Tanzania katika upande wa kusini na kusini magharibi, Uganda upande wa magharibi na Sudan kusini katika upande wa kusini mashariki.
Rais wa kenya huitwa William Ruto na wa Tanzania rais Samia suluhu , Kisha yule wa Uganda ni Yoweri Kaguta Museveni. Kenya hutangamano na Taifa hizi tatu kupitia biashara, elimu na hata masuala ya uvuvi. Naipenda nchi yangu kwasababu Mimi ni mzalendo ni mtu anayependa nchi yake na Yuko tayari kufa kwasababu ya nchi.
Kenya ilipata uhuru mwaka wa elfu moja mia Tisa sitini na tatu , baada ya kupitia mateso ya wazungu.kenya Ina mabunge mawili bunge la kaunti.spika wa bunge la kitaifa anaitwa Moses wetangula . Naibu wa rais nchini kenya anajulikana kama bwana Rigathi Gashagua.Hayati Mzee Jomo Kenyatta ndiye alikuwa rais wa kwanza wa nchi ya kenya.alifuatiwa na hayati Daniel arap moi halafu marehemu mwai kibali , aliyejulikana kama mwanauchumi halisi.hayati Daniel arap moi atakumbukwa kwa kutuletea maziwa ya nyayo .naye mwai kibaki atakumbukwa kwa kutuletea elimu ya bure.
Rais mstaafu uhuru kenya atakumbukwa kwa elimu ya “C.B.C” yaani mtaala ya umilisi, baada ya kuaga elimu ya nane nne nne. Wakati wake mwingi alihusika katika kujenga Barabara. Ni Bora kufahamu pia katika Uongozi wake sare ya polisi ilibadilishwa. Ikiwa samawati ni wakati wa Uongozi wa marehemu rais mwai kibaki mwaka wa elfu mbili na kumi ndipo nchi ya kenya ilipata katika mpya.
Nchi yetu Ina mazingira mazuri ya kupendeza kama vile misitu, mito maziwa, milima na mengine mengi. Mazingira ni vitu ambavyo hutuzunguka. Kwa kweli wakenya wengi hawataweza kusahau profesa Wangari Maathai kwasababu alituhamasisha kupanda miti na kutueleza umuhimu wa miti katika Taifa letu la kenya.
Miti ni dawa kwa binadamu. Tunapata matunda kutoka kwa miti, miti huvuta mvua na pia inazuia mmomonyoko wa udongo. Hii ndio maana Rais William Ruto alitenga siku maalum ya kupanda miti mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu. Kila mwanafunzi alihimizwa kupanda miti katika shule yako.
Nchini kenya waziri wa mazingira anaitwa soipan Tuya.
Serikali yetu tukufu ilipiga marufuku utumiaji wa karatasi za sandarusi ambazo ziliaminika ndizo chanzo kikuu Cha uchafuzi wa mazingira yetu. Tukiishi katika mazingira safi, Ugonjwa wa kuhara na kutapika yaani kipindupindu, utakosekana nchini. Tushirikiane sote kudumisha usafi wa mazingira tunamoishi. Kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Kenya ni nchi yetu tunayoipenda, tuipende na kuilinda milele daima.
Nchi yetu ya kenya Ina vyombo mbalimbali vya mawasiliano kama vile runinga ya citizen, K.T.N, N.T.V na televisheni arobaini na saba. Mkuu wa kituo Cha citizen huitwa S.K. Macharia. Vyombo vya habari husaidia wananchi kujua mambo ambayo hutokea nchini.
Najivunia Bendera yetu ya kenya. Bendera hii Huwa na rangi nne kuu ;nyeusi, husimamia waafrika weusi. Rangi nyekundu huashiria damu iliyomwagika wakati kenya ilipigania uhuru, Rangi ya kijani kibichi husimamia mazingira yetu na hatimaye nyeupe ni usafi w moyo. Wimbo wa Taifa imetungwa kwa lugha mbili kuu, kiswahili na kingereza. Kuna lugha rasmi mbili kiswahili na kingereza na lugha ya ishara.
Bali na mji mkuu wa Nairobi kuna miji mingine ambayo hutambuliwa kama miji mingine ambayo hutambuliwa kama miji mikuu kama vile Nakuru, Kisumu na Mombasa. Taifa la Kenya hutambulika zaidi katika riadha.kuna baadhi ya wanariadha tajika kama vile Faith Kipyegon, Lilian Obiri na mwendazake kelvin kiptum. Kila mwamba Ngoma huvutia na kwake.
Wakenya husifiwa katika tamaduni zao, kama vile wamaasai huvaa shuka na kina dada huvalia shanga shingoni. Utamaduni huu huletea nchi yetu pesa ambazo hutumika kujenga uchumi wa nchi. Barabara za kenya huvutia zaidi kama vile Thika “super high way” Barabara hii husaidia katika kusafi kwa haraka na kuzuia ajali barabarani. Kuna sehemu maalum ambayo hutengewa magari na sehemu ya watu kupita.