7.4 C
London
Friday, November 22, 2024
HomeInternationalKENYAPombe Haramu Yakera Wakaji Muranga na Athari Zake. (Swahili)

Pombe Haramu Yakera Wakaji Muranga na Athari Zake. (Swahili)

Date:

Related stories

Why Africa is Still Poor?

Africa, rich in natural resources and cultural diversity, paradoxically...

Kenya’s Journey Toward a Cashless Economy

Kenya has been at the forefront of the digital...

Mau Mau: Mukami Kimathi’s swansong to a city at war

By Jaclynn Ashly 72 years after the Declaration of Emergency...
spot_imgspot_img
Reading Time: 3 minutes

Pombe ni kinywaji kinacholevya . Katika Gatuzi la Muranga unywaji wa pombe umekuwa na madhara mengi. Wananchi wamekerwa na janga Hilo , hata hivyo serikali imejitolea kupiga Vita pombe hii haramu. Baadhi ya athari ya pombe haramu ni kama ifuatavyo.

Watafiti wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa kuenea zaidi kwa athari mbaya wa ubongo. Kuendelea kunywa kwa pombe unaweza kusabsbisha kupungua kwa uwezo wa kukumbuka .wale ambao hunywa pombe wakati mwingine hupenda kuimba wakati wanatoka klabuni. Wimbo wao kwa Mara nyingi huwa na matusi. Ni Bora tusiwabagua walevi kule kijijini .
Husababisha kifo.
Ilikuwa Jambo la kushangaza katika Gatuzi la Muranga. Paliondokea kizaza ambapo kijana aliyeitwa “Leo mbutu ” alishiriki shindano la kunywa pombe , kisha akapoteza maisha yake. Kisa hicho kilifanyika katika mtaa wa mukanga . Leo mbutu alikunywa glasi tatu kisha akapoteza fahamu alipofikishwa hospitalini .

Matatizo ya moyo.
Pombe huchangia Sana katika kudhoofisha mishipa ya moyo hivyo kupelekea ugonjwa wa “cardiomyopathy ” Jambo hili hutokea wakati ambapo mshipa wa moyo hudhoofika na kushidwa kusukima damu . Wakati damu huganda bila shaka husababisha ugonjwa wa kiharusi. Pia pombe huleta ugonjwa wa kongosho. Ni Bora binadamu aepuke unywaji wa pombe ikiwa hajakuwa mraibu sugu. Matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu, huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi. Waraibu wa pombe huwa na harufu mbaya mdomoni, hii ni kwasababu wengine wao hawapendi kupiga mswaki. Ingawa Kuna walevi ambao hawakosi kuenda kanisani kuomba mungu.

Matatizo ya uzazi.
Uraibu wa pombe haibagui jinsia ya kike au kiume . Dhahiri shairi wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume na wanawake hushindwa kushika mimba kirahisi. Jamii hutengana kulingana na matatizo ya pombe. Kwasababu jinsia hivi mbili husahau majukumu yao ya familia na kufanya watoto kuteseka. Unywaji wa pombe hufanya mtu kupoteza heshima katika jamii na pia kupoteza kazi yake. Hii hutokea mtu anapochelewa kazi Kila siku. Ni Bora kutunza kazi zetu , kwasababu tunapa mapato kuendeleza jamii.

Matatizo ya ini.
Watu wengi hupenda kunjwa pombe vilabuni au nyumbani kwao kwa njia ya kujistarehesha na kupunguza mawazo yao. Ajabu ni kwamba pombe huleta matatizo ya ini pamoja na majeraha ya ajali. Dereva huendesha gari kwa kasi bila kuzingatia Sheria za barabarani hatimaye abiria huangamia na kupoteza maisha yao

Ukatili na ubakaji.
Kule kijijini pombe harama imesababisha ukatili , kujinyonga , ubakaji na ugomvi. Maafa haya yote hutokana na vijana kukosa maadili na mwelekeo Bora. Wengi wao hunywa pombe ili kusahau matatizo yao ya maisha wanapofanya hivyo huchangia ukosefu wa usalama kijijini. Kina mama na watoto ndio hujipata taabani. Kwa Mara nyingi wao hubakwa na kupata uja uzito.

Mapenzi kiholela.
Pombe haramu hufanya waraibu kufanya mapenzi bila Kinga au mapenzi nje ya ndoa. Mapenzi hii huleta magonjwa ya zinaa kama ukimwi. Kule Muranga watu nne walifariki baada ya kunywa pombe ya kitamaduni. Mke wa mmoja wa marehemu alihusishwa na pombe hiyo. Ingawa sherehe huleta watu pamoja , sherehe hiyo ilibadilika na kuwa karaha. Jamaa hao wa familia walikuwa wanasherehekea kufunguliwa kwa nyumba . Leo ni Leo asemaye kesho ni mwongo , pombe hiyo ilidaiwa kuwa na sumu na kuleta kilio Cha pekee.

Pombe ya “Muratina ” imewapokonya wengi wapendwa wao . Unywaji wa pombe ulichangia kwa kiasi kikubwa uvutaji wa sigara, mraibu wa pombe hakosi sigara mdomoni. Pombe huletea familia umasikini chungu tele. Wanaume husahau jukumu yao na kuachia ulezi kina mama . Si rahisi wao kununulia watoto chakula na mavazi. unywaji wa pombe hupunguza uwezo wa seli nyekundu za damu kusafirisha oksijieni ya kutosha na kupelekea ugonjwa wa anaemia.

Ni dhahiri shairi kuwa vinjwaji vilivyotengenezwa kwa matunda bila kilevi ni Bora zaidi kwa afya . Wengine huamini kuwa pombe huboresha maswala ya uzazi huku wengine wakiamini pombe huathiri maswala ya uzazi. Hongera naibu wa rais bwana Gashagua kwa kupiga Vita uraibu wa pombe mjini Muranga.

About The Author

Subscribe

- Never miss a story with notifications

- Gain full access to our premium content

- Browse free from up to 5 devices at once

Latest stories

spot_imgspot_img