Kujipumzisha si anasa, bali ni lazima kwa kila mfanyikazi na wanafunzi kwani Wana haki ya kupumzika baada ya kazi . Kupumzika baada ya kuchapa kazi kwa muda utaboresha utendaji kazi wako. Zifuatazo ni faida ya Likizo Kwa Wanafunzi pamoja na wafanyikazi. Utendaji bora wa kazi .Watu wanaoenda likizo wanafanya kazi zaidi na kila mara Wana nafasi kubwa zaidi ya kupandishwa cheo na kufanikiwa, kuliko watu wasioenda likizo. Ikiwa utajipatia muda wa kupumzika baada ya kuchapa kazi kwa muda, ni thibitisho wa utendaji bora wa kazi.
Kupunguza msongo wa mawazo, si ajabu kusikia kwamba kuwa na msongo wa mawazo ni dalili ya kuchapa kazi kupita kiasi .Msongo wa mawazo huchangia magonjwa kadha kama vile Ugonjwa wa moyo , kansa , magonjwa ya mapafu, ajali , magonjwa ya ini na wakati mwingine kutaka kujitoa uhai bila sababu kuu. Likizo husaidia kuongeza ubunifu shuleni au kazini.
Wengi wetu tumeona wafanyikazi wakirudi kutoka likizo akiwa amebadilika kabla ya kwenda likizo.Mtu akienda likizo huwa anarudi na mawazo mapya na msisimko wa mawazo.Ubongo ukipumzika utapokea taarifa mpya na tena kwa ukamilifu.Likizo husaidia mwanafunzi kuwa na ujuzi na matokea mapya , ni bora kifanya mazoezi Wakati wa likizo, watu husafiri sehemu mbalimbali za nchi lengo kuu ni kupumzika. Wawaache watoto wapumzike, kusoma masomo zaidi ya saba kila siku ya wiki sio kitu rahisi, akiwa likizo mwache angalie au atazame televisheni, mwache acheze , mwache alale , unachoweza kumpa moto kama zawadi , mwache mtoto afurahia likizo yake, ikiwa mtoto hataweza kusafiri wakati wa likizo, Wacha Watoto wajifunze majukumu ya nyumbani na nje ya darasa.
Wakati wa likizo masomo kama muziki, kuogelea, kuimba, kucheza mpira na kupiga kinanda , inaweza kuwa fursa kwa mtoto kunoa kipaji chake wakati likizo. Likizo ni bora zaidi kwa wanafunzi,muda huu wanafunzi huongeza maarifa hasa ya teknolojia na mambo mengine yanayohusu mtaala ili kuongeza ushindani na hufaulu wakirudi shuleni.
Mara nyingi watoto hulazimika kuamka mapema ili kuwahi madarasa haya,ratiba ambayo haitofautiani sana na miezi wanayokuwa masomoni.Hali hii huacha wadau wa elimu wakiwa na maswali mengi kinywani mwao .Hata hivyo wao hupatiwa maswali mengi ya ziada, likizo ni bora kwasababu wataweza kupumzisha akili zao na kutangamana na marafiki wenzao kutoka shule mbalimbali kote nchini.
Sio lazima likizo iwe ya gharama kubwa au kwa muda mrefu ili iwe na faida .Ni bora uende kwenye likizo ya wikendi sehemu isiyo na gharama kubwa badala ya kutokwenda kabisa. Lengo kuu ni kujitoa kabisa katika maisha yako ya kila siku.Tusisahu kuwa wakati wa likizo wanafunzi huongeza maarifa Kisha wanatembelea sehemu za Sanaa na utamaduni.
Wanafunzi wakiwa likizoni wao huongeza furaha zaidi.Sayansi imethibitisha kuwa ukiwa likizoni, mwili wako unatoa homoni ya furaha ya “serotonin” hii inapumzisha viwango vya cortisol . Mwisho wa siku , homoni nzuri zaidi zinazalishwa ndani ya mwili wako na kuchangia mtazamo wako wa kuimarika . Kama unaendesha biashara, nenda likizo ili ujue biashara mbalimbali ya kuendesha biashara na pia ufunzwa jinsi ya kutumia wakati wako wakati likizo.
Ukosefu wa mapumziko siyo kitu kizuri hasa kwa ukuaji wa akili ya mtoto na wengi wanaoshindwa kulielewa hilo , wakidhani shule ndio kitu Cha pekee ambacho mtoto anatakiwa kuwaza mara kwa kwa mara . Wazazi wanatakiwa kuelewa ujuzi wa watoto wao . Wanafunzi wasipatiwe elimu ya darasani pekee, kwani, kwa mfano ikiwa Messi asingekuwa mcheza mpira mzuri, asingekuwa mwerevu, tunafikiri watoto wakipata asilimia mia moja au A ni kufahamu elimu ndani ya darasa.
Licha ya mfumo wa elimu kuweka kipindi cha likizo, ni jambo la kuvunja moyo , ukisikia kuwa bado Kuna baadhi ya wazazi ambao huwapeleka watoto wao katika masomo ya ziada.Jambo hili ni njia moja ya kuwatesa Watoto wao.
Waziri wa elimu Ezekiel Machogu, amewapatia wanafunzi likizo ya wiki nne. Hii ni ishara tosha kuwa likizo ni muhimu kwa walimu pamoja na wanafunzi kupumzika nyumbani.Mwili wa binadamu unahitaji muda wa kutiliza mawazo kidogo si masomo kila wakati .Ni jukumu la serikali kutoa mazingira salama ya watoto kuchezea.
Likizo husaidia kuongeza ubunifu shuleni au kazini.Wengi wetu tumeona wafanyikazi wakirudi kutoka likizo wamebadilika kabla kuenda likizo .Mtu akienda likizo huwa anarudi na mawazo mapya na msisimko wa ubongo ukipumzika utapokea taarifa mpya na tena kwa ukamilifu.Likizo husaidia mwanafunzi kuwa na ujuzi na matokea mapya, hii ni kwasababu amefanya mazoezi .Ni vyema pia kutenga muda wetu wa likizo kumtukuza mwenyezi Mungu na kuboresha mazingira yetu kila Wakati.